Iraq ya kaskazini inamchango wake katika muonekano wa Arubaini: Mawakibu za maombelezo za Arbiil katika mji mtukufu wa Karbala…

Maoni katika picha
Wapenzi wa bwana wa mashahidi (a.s) kutoka katika Dini na madhehebu tofauti wanaendelea kumiminika katika mji wa Karbala, jambo hili tumezowea kuliona kila mwaka ufikapo msimu wa ziara ya Arubainiyya, Imamu Hussein (a.s) sio wa Dini au madhehebu moja peke yake, kwani linapo tajwa jina lake (a.s) hukumbukwa misingi ya kibinaadamu aliyo ipigania yeye pamoja na watu wa nyumbani kwake na maswahaba wake.

Kundi kubwa la watu wa Arbiil na miji ya jirani yake limekuja kutoa pole kwa mjikuu wa Mtume na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ziara ya Arubainiyya, hakika imani zao na mapenzi ya Mtume Muhammad na watu wa nyumbani kwake (a.s) ndio yamewasukuma kuja katika mji mtukufu wa Karbala.

Watu hawa kutoka katika mji wa Arbiil wameonyesha furaha kubwa sana kwa kushiriki katika ziara hii, wakabainisha kua Hussein ni moja ya nguzo muhimu zinazo waunganisha raia wa Iraq, hakika yeye ni nguzo ya umoja wao, kwa sababu mambo aliyo yafanya katika uislamu ni sawa na hema linalo mfunika kila mtu anayetaka mafanikio na umoja, pia mafundisho yake hayawahusu waislamu peke yao, bali yanahusu wanaadamu wote, na ataendelea kua jua ling’aalo vizazi na vizaji, wairaq wote ni watoto wa Hussein, wamejifundisha ushujaa wa kupambana na maadui wa mwisho walio kuja kuiteka Iraq kutoka kwake, na wakashinda kwa baraka zake.

Tunapenda kusema kua mji wa Karbala katika siku hizi unapokea mamilioni ya watu kutoka kila sehemu ya Dunia, wanaokuja kumzuru Abu Abdillahi Hussein (a.s) na kuomboleza msiba wake pamoja na kuhuisha utiifu wao kwake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: