Zaidi ya maukibu (3000) zimetoa huduma kwa mazuwaru katika mji wa Basra…

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kimetangaza kua mwaka huu maukibu (3563) zilizo sajiliwa rasmi katika kitengo cha mawakibu, zimetoa huduma kwa mazuwaru wa Arubaini, bila kuhesabu maukibu zingine pamoja na nyumba za watu binafsi zilizo tumika kutoa huduma bila usajili rasmi na zingine zilizopo katika maeneo ya mbali kabisa sehemu za mipakani sambamba na zile maukibu za kuhama hama, ambazo hutoa huduma zaidi ya sehemu mujo zikifuata muelekeo wa mazuwaru kwa ajili ya kutafuta thawabu zaidi.

Kitengo kikifanua kua: “Maukibu hizo zimesambaa katika barabara zote zinazo tumiwa na mazuwaru katika mkoa wa Basra, pamoja na kuwepo kwa wingi zaidi katika sehemu zenye mazuwaru wengi”.

Wakabainisha kua: “Mwaka huu misafara ya mazuwaru ya kwenda Karbala ilianza mapema, mawakibu za kutoa huduma haziishii kutoa huduma peke yake, bali zinatoa ushirikiano mkubwa kwa vikosi vya ulinzi na usalama vilevile, baada ya kuisha misafara ya mazuwaru katika mkoa huu, wahudumu wa mawakibu nao wataanza safari ya kwenda Karbala ili wapate utukufu mara mbili, utukufu wa kutoa huduma na utukufu wa kufanya ziara”.

Kumbuka kua kuna utaratibu maalumu ulio pangwa katika utowaji wa huduma pamoja na watu wa usalama na afya, kila sekta imefanya kila iwezalo katika kufanikisha utendaji wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: