Huduma ya mara hii zinatolewa kwa kaswida za kimashairi…

Maoni katika picha
Barabara ya kuelekea katika Kaaba ya mapenzi Karbala tukufu, kila sehemu utakutana na bango lenye maana elfu (nyingi), lakini ukarimu ndio bango kuu, hakika ni ukarimu wa Husseini katika njia ya Husseini.. lakini tulipo fika pembezoni mwa mkoa wa Samaawa wilaya ya Khadhar, tulikutana na maukibu iitwayo Imamu Hussein (a.s), iliyo kua na huduma tofauti kabisa.

Maukibu hiyo ilikua inatoa huduma kwa kaswida za kimashairi, kundi la watu wa makabila walikua wamesimama barabarani na kuwapokea mazuwaru kwa kuwaimbia kaswida za kimashairi yanayo mpa hamasa zaairu pamoja na nguvu ya kuendelea na safari, kaswida hizo zilikua zinahusu utukufu wa Ahlulbait (a.s) na misimamo yao ambayo imebakiza heshima ya ubinaadamu milemile na milele.

Tulipo wauliza kuhusu utowaji wa huduma zao, walijibu kua: “Hakika hii ndio njia sahihi ya uadilifu na inayo enzi utamaduni wa mwanaadamu, kwa hiyo sisi tunahuisha utamaduni wa kaswida za kimashairi ambao ndio urithi wa kihistoria wa waarabu, tunataka kuuhuisha na kuurithisha kizazi baada ya kizazi”.

Tukapita na kuwaacha wanaimba: (Mdhamini wa tiba kubwa muache aendelee kudhamini).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: