Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mkoa wa Muthanna chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imefungua vituo vya kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani.
Mkoa wa Muthanna unashuhudia uwepo wa vituo vingi vya utowaji wa elimu katika barabara zinazo tumiwa zaidi na watu wanaokwenda kumzuru bwana wa mashahidi (a.s), katika vituo hivyo kunafundishwa usomaji sahihi wa surat Fat-ha pamoja na sura zingine fupi fupi na nyeradi za swala zinazo pelekea kukamilika kwa faradhi hito tukufu.
Kumbuka kua Maahadi imeweka vituo hivyo katika mkoa wa Muthanna, Baabil, Najafu pamoja na Karbala tukufu, katika barabara kuu zinazo elekea Karbala, miongoni mwa barabara hizo ni: (barabara ya Karbala, Bagdad / Karbala, Baabil / Karbala, Najafu), vituo hivyo vinaendeshwa na matawi ya Maahadi yaliyopo katika mikoa hiyo, kumbuka kua vituo hivyo vinatoa huduma kwa mwaka wa nne mfululizo katika miji hiyo.
Mazuwaru wametoa shukrani nyingi kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia Maahadi ya Qur’ani kwa kuendesha mradi huu muhimu, kwani umejikita katika kufundisha visomo muhimu vya swala ambavyo ndio sharti la kusihi kwa faradhi hiyo adhim.