Kwenye mpaka wa mkoa wa Dhiqaar: Zaidi ya maukibu (3500) zinatoa huduma kwa mazuwaru wa Arubaini…

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya cha Ataba mbili tukufu kimetangaza kua: “Idadi ya maukibu zilizo shiriki kutoa huduma kwa mazuwaru wa Arubaini katika mpaka wa mkoa wa Dhiqaar zimefika (3570) zilizo sajiliwa, mbali na mamia ya Husseiniyya na nyumba za watu zinazotoa huduma bila usajili”.

Akaongeza kua: “Kuna mawakibu zinatoa huduma katika mikoa mingine kwenye barabara zinazo tumiwa na mazuwaru, sambamba na mawakibu zilizopo katika mkoa wa Karbala pamoja na kwenye barabara zinazo elekea mkoa huo”.

Wakafafanua kua: “Hakika mawakibu zipo katika kila njia inayo tumiwa na mazuwaru, na zinakuwepo kwa wingi katika barabara zinazo tumiwa na idadi kubwa ya mazuwaru”.

Wakabainisha: “Mwaka huu misafara ya kuelekea Karbala ilianza mapema zaidi, na mawakibu za kutoa huduma haziishii kuwahudumia peke yake, bali zinatoa ushirikiano mkubwa kwa vikosi vya ulinzi na usalama, na baada ya kuisha misafara ya mazuwaru katika mkoa huu, wahudumu wa maukibu hizi wataondoka kwa miguu kuelekea Karbala ili wapate utukufu mara mbili, utukufu wa kutoa huduma na utukufu wa kufanya ziara”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: