Kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa wito kwa vyombo vya habari vinavyo penda kurusha matukio ya ziara ya Arubaini wafike ofisini na kukamilisha utaratibu ulio wekwa kwa ajili ya kurahisisha utendaji wao na uingiaji wao katika Ataba mbili na katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, pamoja na kuwapa vitambulisho maalumu, yamesemwa haya na makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Aqiil Abdulhussein Yasiri.
Akaongeza kua: “Kwa ajili ya kuratibu kazi za waandishi wa habari katika ziara ya Arubaini kwa namna itakayo wezesha kurusha picha halisi ya ziara hii tukufu, bila kuwepo usumbufu wowote, kitengo kimeweka utaratibu wa kazi, unaanzia kupokea maombi kutoka kwa chombo cha habari kinacho taka kurusha matukio haya, halafu jina la kituo hicho linaandikwa katika orodha maalumu ya vyombo vya habari pamoja na majina ya waandishi wa habari na aina ya habari zao (Luninga – gazeti – redio na zinginezo) na majina ya watu wanakao fanya kazi hiyo, kisha wanapewa vitambulisho ambavyo mfano wa vitambulisho hivyo wamepewa pia Atabatu Husseiniyya na uwanja wa eneo la katikati ya haram mbili tukufu, ili kuwarahisishia utendaji wao chini ya taratibu tulizo kubaliana”.
Kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa maelekezo maalumu kwa waandishi wa habari wanaotaka kurusha matukio ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) yatatangazwa baadae.