Kitengo cha maadhimisho, mawakibu na vikundi vya Husseiniyya chatoa ratiba ya kuingia kwa mawakibu za zanjiil na chahimiza iheshimiwe…

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho, mawakibu na vikundi vya Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya ambacho kinawajibika kuratibu uingiaji wa mawakibu zinazo omboleza arubaini ya Imamu Hussein (a.s), kimetoa ratiba inayo onyesha muda wa mawakibu na vikundi vya husseiniyya kuingia katika maeneo matakatifu, na kimesisitiza kuheshimiwa ratiba hiyo, fahamu kua ratiba hiyo inaanzoia muda wa kuondoka katika jukwaa lililopo kwenye barabara ya Kibla ya Imamu Hussein (a.s) hadi kuingia katika Atabatu Husseiniyya tukufu na kuelekea katika Atabatu Abbasiyya na kuhitimishia huko msafara wa maukibu, tunatarajia kutoenda kinyume na utaratibu huu uliotajwa kwa ajili ya kumtumikia Imamu Hussein (a.s) na mazuwaru wake watukufu, Mwenyezi Mungu atuwezeshe.

15 na 16 Safar 1440h.

  • 1- Kuingia mawakibu zote kutoka katika mkoa wa Dhwa’an.

16 Safar 1440h.

  • 1- Kuanzia saa 1 hadi saa 3 asubuhi kuingia mawakibu kutoka mkoa wa Naswiriyya na wilaya zake.
  • 2- Kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 5 Adhuhuri kuingia mawakibu za Kadhimiyya tukufu.
  • 3- Kuanzia saa 7 hadi saa 8 baada ya Adhuhuri kuingia mawakibu za Najafu na wilaya zake.
  • 4- Kuanzia saa 8 hadi saa 10 Alasiri kuingia mawakibu za Diwaniyya na wilaya zake.
  • 5- Kuanzia saa 1 hadi saa 3 usiku kuingia mawakibu za mkoa wa Misaani.
  • 6- Kuanzia saa 3 hadi saa 5 usiku kuingia mawakibu za mkoa wa Diyala.

17 Safar 1440h.

  • 1- Kuanzia saa 1 hadi saa 3 asubuhi kuingia mawakibu za mkoa wa Basra na wilaya zake.
  • 2- Kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 5 adhuhuri kuingia mawakibu za mkoa wa Baabil na wilaya zake.
  • 3- Kuanzia saa 7 Adhuhuri hadi saa 9 Alasiri kuingia mawakibu za mkoa wa Waasitu na wilaya zake.
  • 4- Kuanzia saa 9 hadi saa 11 jioni kuingia mawakibu za mkoa wa Karkuuk na Nainawa pamoja na wilaya zake.
  • 5- Kuanzia saa 1 jioni hadi saa 3 usiku kuingia mawakibu za mkoa wa Samaawa na wilaya zake.
  • 6- Kuanzia saa 4 hadi saa 5 usiku kuingia mawakibu za mkoa wa Swalahu Dini na wilaya zake.
  • 7- Kuanzia saa 5 hadi saa 6 usiku kuingia mawakibu za mkoa wa Naswiriyya na wilaya zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: