Darul-Kafeel yachapisha zaidi ya nakala milioni za ziara ya Arubaini…

Maoni katika picha
Miongoni mwa taasisi za kielimu zilizo jitolea kuwahudumia mazuwaru wa Arubaini ni kituo cha uchapishaji cha Darul-Kafeel, kimeandaa machapisho maalumu kwa ajili ya mazuwaru wa Arubaini, kimechapisha zaidi ya nakala milioni moja na kuzigawa kwa wanufaika.

Machapisho hayo yanaubora wa hali ya juu, wino mzuri, karatasi za kisasa, hati yenye muonekano mzuri na mengine mengi yanayo endana na utukufu wa ziara hii.

Watumishi wa kituo hicho wamefanya kazi kubwa ya kuandaa machapisho ya aina mbalimbali kwa ajili ya ziara ya Arubaini, ambayo ni (folda, vijitabu, vipeperushi, na cd), machapisho hayo yamesheheni maelekezo na nasaha za Dini na mambo ya kisheria, Fiqhi na Aqida, pamoja na vipeperushi vya kufundisha usomaji sahihi wa surat Fat-ha pamoja na michoro ya ramani kwa ajili ya kumwongoza zaairu wa Arubaini, bila kusahau ziara maalumu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika siku ya Arubaini ambayo imeandikwa kwa lugha tofauti (Kiarabu, Kiingereza, Kifarsi na Kiswahili).

Kumbuka kua utowaji wa huduma wa Atabatu Abbasiyya tukufu hauishii katika vitengo vyenye uhusiano wa moja kwa moja na mazuwaru, bali kuna vitengo na taasisi zilizo chini ya Ataba tukufu zinafanya kazi kubwa ya kuwahudumia mazuwaru, na miongoni mwao ni kituo hiki cha uchapishaji na usambazaji cha Darul-Kafeel.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: