Sayyid Sistani awahusia mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) Allah Allah katika swala…

Maoni katika picha
Miongoni mwa usia na maelekezo yaliyo tolewa na ofisi ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Ayatullahi Sayyid Ali Husseini Sistani kwa watu wanaokwenda kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), jambo alilo sisitiza sana ni kuswali kwa wakati, kwani swala ndio ibada aipendayo zaidi Mwenyezi Mungu mtukufu, kumzuru Imamu Hussein (a.s) ni mustahabu lakini swala ni wajibu, swala inakuweka karibu na Mwenyezi Mungu mtukufu na kwa kupitia Imamu Hussein (a.s), aliyasema hayo alipo kua anajibu swali la waumini waliokwenda kumtembelea na wakamuomba awahusie kuhusu tukio hili ili waweze kunufaika zaidi, maelezo hayo yameandikwa katika mtandao rasmi ya ofisi ya Mheshimia nasi tunayanukuu kama yalivyo:

(Allah Allah katika swala hakika -swala kama ilivyokuja katika hadithi- ni nguzo ya Dini na ngazi ya waumini, ikikubaliwa na ibada zingine zitakubaliwa na ikikataliwa na ibada zingine zitakataliwa, inatakiwa iswaliwe mwanzoni mwa wakati wake, hakika ndio ibada aipendayo zaidi Mwenyezi Mungu mtukufu, na huitikia haraka anapoompwa katika swala, haitakiwi kujishughulisha na jambo lingine mwanzoni mwa wakati wake, hakika swala ndio ibada bora zaidi, imepokewa kutoka kwa kwao (a.s): (Hatapata shifaa yetu anaye puuza swala). Imepokewa kutoka kwa Imamu Hussein (a.s) namna alivyo ipa umuhimu swala katika siku wa Ashura, alimwambia yule aliye mkubusha mwanzoni mwa wakati wa swala: (Umekumbuka swala Mwenyezi Mungu akujaalie uwe miongoni mwa wanaoswali na wakumbukao) Imamu (a.s) aliswali katika uwanja wa vita huku akishambuliwa kwa mishale).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: