Ambayo hayajafikiwa na watangazaji wa Arubaini: ni matembezi na huduma za Husseiniyya zinazo fanyika katika jangwa la Iraq…

Maoni katika picha
Makundi makubwa ya watu yanaendelea kumiminika katika mji mtukufu wa Karbala katika matembezi yasiyo kua na mfano hapa duniani, wanatumia njia zote, za zamani na mpya kutoka katika miji na majangwani, kuna njia zinaanzishwa na kukomazwa na miguu ya watembeaji wasio ogopa jua wala mvua, utakuta msafara unaendelea kutembea muda wote wala hakuna wakati ambao unaacha kutembea, vipi wataacha kutembea wakati lengo lao kuu nia kiini cha uhai na njia ya uhuru!! Vyombo vya habari vimejitahidi kutangaza matembezi haya kwa walimwengu lakini vimesahau sehemu ya matembezi hayo, sehemu ya watu wanaoishi majangwani na misafara yao inaanzia huko huko jangwani kuelekea Karbala, sambamba na kuwepo kwa mawakibu za kutoa huduma zilizo andaa sehemu za kupumzika mazuwaru huko huko katikati ya jangwa.

Mtandao wa kimataifa Alkafeel unakuletea matembezi hayo ya watu wa jangwani ambao wametembea umbali wa kilometa (1500) kutokea katika mpaka wa Kuwait, Saudia na Iraq, katika mji wa Garanji Abadawiyya kwenye mpaka wa mkoa wa Basra, kisha wakaelekea katika mji wa Takhalidi, Aadin, Baswiyya, Salmaan, Mumliha hadi katika mpaka wa mkoa wa Muthanna, kwa kupitia njia inayoonganisha mikoa ya kusini magharibi mwa Iraq, hadi wanawasili katika mji mtukufu wa Karbala kwa kupitia jangwa la Najafu.

Kamera ya Alkafeel inakuletea msafara huo wa mazuwaru wa Arubaini walio tembea kwa miguu hadi Karbala tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: