Sayyid Sistani awahutubia mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s): Allah Allah katika Ikhlasi…

Maoni katika picha
Miongoni mwa usia na maelekezo yaliyo tolewa na ofisi ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Ayatullahi Sayyid Ali Husseini Sistani kwa watu wanaokwenda katika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), jambo alilo sisitiza sana ni Ikhlasi, kwa sababu thamani ya ibada yeyote inatokana na Ikhlasi yake kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, hakika Mwenyezi Mungu hapokei ibada ispokua itakayo ambatana na Ikhlasi na ikatakasika na kumuomba asiyekua yeye, aliyasema hayo wakati akijibu swali kutoka katika kundi la waumini wanaokwenda ziara na walio omba nasaha zake ili waweze kupata faida zaidi, maelezo haya yanapatikana katika toghuti ya ofisi yake na sisi tunanukuu kama yalivyo:

(Allah Allah katika Ikhlasi, hakika thamani ya ibada ya mwanadamu na baraka zake inatokana na Ikhlasi yake kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, hakika Mwenyezi Mungu hakubali ibada yeyote ispokua iliyo fanywa kwa Ikhlasi na ikatakasika na kumuomba asiyekua yeye. Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) wakati waislamu walipo hamia Madina alisema: (Hakika aliye hama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi kuhama kwake kutakua ni kwa ajili ya hao, na aliye hama kwa ajili ya kutafuta Dunia basi kuhama kwake kutakua ni kwa ajili hiyo, hakika Mwenyezi Mungu huongeza thawabu katika tendo la ibada kutokana na kiwango cha Ikhlasi hadi zinafika mia saba na Mwenyezi Mungu humuongezea amtakae.

Mazuwaru wanatakiwa kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi katika safari yao, na kuwa na Ikhlasi katika kila hatua na kila jambo, na watambue ya kua Mwenyezi Mungu hakuna neema kubwa aliyowapa waja wake zaidi ya Ikhlasi katika itikadi, vitendo na kauli, hakika ibada isiyokua na Ikhlasi huisha pamoja na uhai wa duniani, na yenye Ikhlasi hubakia milele na milele hapa duniani na baada ya kufa).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: