Kwa ajili ya kujibu maswali ya mazuwaru ya kifiqhi na kutoa maelekezo ya kisheria, kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu katika ratiba yake na mkakati wake katika kipindi cha ziara ya Arubaini kimeweka vituo vya kujibu maswali ndani ya uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, ambao kazi yao kubwa ni kujibu maswali na kutoa maelekezo kwa mazuwaru.
Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha Dini Shekh Swalahu Karbalai kwa mtandao wa Alkafeel, amesema kua: “Vituo hivyo ni sehemu ya mkakati ulio wekwa na kitengo hiki katika kipindi cha ziara ya Arubaini ambacho ni kipindi muhimu kitablighi, hali kadhalika ratiba hiyo inaingia katika mradi wa tabligh za kihauza unao simamiwa na hauza tukufu, jukumu kubwa la vituo hivyo ni kujibu maswali ya mazuwaru ya kifiqhi na kiaqida na mengineyo pamoja na kufafanua mambo mbalimbali yenye uhusiano na zaairu”.
Akabainisha ku: “Kitengo kimeteua jopo la wasomo wa Dini kwa ajili ya kusaidiana na watumishi wa kitengo katika kipindi hiki, na wanafanya kazi saa zote”.