Kuanza kwa moja ya hatua za maombolezo ya Arubaini: Mawakibu za zanjiil zahuisha ahadi ya kiapo cha utii na utekelezaji…

Maoni katika picha
Ilipo ingia asubuhi ya Ijumaa (16 Safar 1440h) sawa na (26 Oktoba 2018m), mawakibu za kuomboleza (zanjiil) zilianza kumiminika katika malalo mawili matakatifu ya Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), ikiwa ni hatua mpya ya uombolezaji wa Arubaini ziliingia maukubu moja baada ya nyingine, kutoka katika mikoa ya Iraq kama ilivyo pangwa katika ratiba ya tukio hili litakalo dumu siku mbili, wanatoa pole kwa Imamu Hujjat bun Hassan (a.f) huku wakipiga vifua vyao na kutokwa machozi na kujikumbusha mauwaji ya Twafu pamoja na kuhuisha utii wao kwake na utayari ya kumnusuru bwana wa mashahidi (a.s).

Matembezi ya maukibu yanaanzia katika barabara ya Kibla ya Imamu Hussein (a.s) na kuelekea katika uwanja wa haram yake tukufu, huku wanaimba kaswida za huzuni kutokana na kumbukumbu hii ya Arubaini ya bwana wa vijana wa peponi (a.s), kisha baada ya hapo wanaelekea katika uwanja wa haram ya ndugu yake jemedari wa Twafu na mbeba bendera yake Abulfadhil Abbasi (a.s) wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu huku wanajipika vifua hadi wanafika katika kaburi la bwana wa maji, baada ya kufika hapo wanalia sana na kuimba kaswida za huzuni kutokana na msiba mkubwa uliopata umma wa kiislamu.

Ali Kaadhim Ankabiy ambaye ni mmoja wa wajumbe wa maukibu ya Abdullahi Radhii itokayo katika kijiji cha Ankabiyya kitongoji cha Khaalisu katika mkoa wa Diyala ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tumetembea mfululizo bila kupumzika kwa muda wa siku kumi na moja tukija Karbala kutoa pole kwa Swahibu Asri wa Zamaan Imamu Mahdi (a.f), sisi tunayachukulia matembezi haya sawa na utambulisho wetu unao thibitisha kua ni wafuasi wa Imamu Hussein na tunawatawalisha watu wa nyumba ya Mtume (a.s), ambao ndio msingi wa utukufu, tunajitahidi sana kuadhimisha alama za Mwenyezi Mungu katika uhai wetu”.

Kumbuka kua kitengo cha mawakibu na maadhimisho ya Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimesha andaa ratiba ya uingiaji wa mawakibu hizi, inayo onyesha sehemu ya kuanzia matembezi njia watakazo pita na sehemu ya kumalizia pamoja na muda unaotakiwa kutumiwa na kila maukibu kwa namna ambayo haitazuwia harakati za mazuwaru wengine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: