Kwa macho yao: Pamoja na uzee wake hajaacha yale aliyokua akiyafanya miaka ya nyuma…

Maoni katika picha
Ni mpenzi wa kutembea kwenda kwa Hussein toka zamani, tangu ilipo kua njia ya Misimiyya ndio njia pekee ya kujikinga na unyanyasaji wa utawala uliopita, anapita katika njia inayo mkumbusha safari zake za zamani.

Anaenzi mwenendo unaofatwa na mazuwaru wa Sayyid Shuhadaa kwa kuingia katika njia za watembea kwa migii akiwa anajihakikishia pepo kwa kila hatua anayo piga, bibi (Sakina Abbasi) amesafiri kutoka kusini ya mto wa Furat na kuelekea katika mji wa Karbala, akikusudia kutekeleza ahadi aliyo weka kwa bibi Zaharaa (a.s) hakuwahi kuhalifu ahadi yake hata baada ya kufikisha umri wa zaidi ya miaka themanini.

Wala azma yake haija vunjika kutokana na watoto wake walio pata shahada (walio uwawa) katika njia ya Hussein, amani iwe ndani ya moyo wako ewe mama wa wairaq, ukiwa pamoja na mwanao unakwenda kufanya ziara ya Arubaini, amani ienee katika uzee wako mtukufu ewe bibi mwenye subira.

Kumbuka kua mradi wa (kwa macho yao) ni mradi wa kiutangazaji unaofanywa na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, unalenga kukuletea picha halisi ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein kupitia jopo la waandishi wa habari wa kiarabu na kiajemi kutoka vyombo tofauti vya habari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: