Ofisi ya wanawake ambayo ipo chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu imezindua maukibu ya kutoa maelekezo kwa mazuwaru wa kike wanaokuja kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kumbukumbu ya Arubaini, maukibu hiyo ipo katika jengo lililo kua likijulikana kama la Ummul Banina (a.s) na sasa lajulikana kama Chuo kikuu cha Al-Ameed katika barabara ya (Najafu/Karbala).
Kiongozi wa ofisi ya wanawake bibi Asmaa Ra’adu Abadiy ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kwa kua tunaishi katika siku za huzuni kubwa ya kumbukumbu ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) na kutekwa familia yake, tumeweka utaratibu unao endana na mazingira, hii ikiwa ni mara ya kwanza, tunatarajia kuboresha zaidi miaka ijayo, na tutaangalia namna ya kuongeza shughuli baada ya utafiti na uchunguzi wa kina, ili maukibu hii iwe na vipengele kadhaa, zikiwemo shughuli za kielimu, kiutamaduni, nadwa na mashindano ya kielimu na maonyesho ya vitabu, maukibu ya wanawake pembezoni ya Hussein (a.s), itakua na vipengele vingi kikiwepo cha usomaji wa dua ya Nudba katika siku za Ijumaa na visomo vya Qur’ani kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Twafu na mashahidi wa jeshi la serikali pamoja na Hashdi Sha’abi, sambamba na kufanya majlisi za kuomboleza zitakazo hutubiwa na watumishi wa ofisi ya wanawake pamoja na kuweka kipengele cha filamu”.
Akaendelea kusema: “Hakika ofisi ya wanawake imejiandaa kutumia uwezo wake wote kwa ajili ya kufanikisha shughuli za maukibu ya wanawake pembezoni ya Hussein (a.s), bila kusahau harakati hii ipo chini ya ratiba ya Arubaini iliyo andaliwa na ofisi ya wanawake kwa jina la (wanawake pembezoni ya Hussein –a.s-), iliyo anza kutekelezwa mwezi tisa Safar na itaendelea hadi siku ya Arubaini ya bwana wa mashahidi (a.s)”.
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imeimarisha ulinzi na usalama pamoja na kuboresha utowaji wa huduma kwa mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), na imewapa nafasi kubwa mazuwaru wa kike ya kuhudumiwa na wanawake wenzao.