Uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kumbi zilizo chini ya Ataba tukufu zafurika watu wanaoswali…

Maoni katika picha
Harakati ya Imamu Hussein (a.s) imebeba ujumbe wa haki na kubadilisha tabia za watu, kutokana na kuongezeka kwa mafungamano yao na Mwenyezi Mungu mtukufu kunako dhihirika katika utekelezaji wa swala, pamoja na ongezeko kubwa la watu wanaokuja kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s). Uwanja mtukufu wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na maeneo yote ambayo yapo chini ya Atabatu Abbasiyya pamoja na vituo vilivyopo katika njia zinazo ingia Karbala maeneo yote hayo yameshuhudia makundi makubwa ya watu wanaoswali.

Mazuwaru wanaonekana kuwa na shauku kubwa ya kuswali swala za faradhi kwa jamaa zinazo ongozwa na Masayyid pamoja na Mashekh watukufu kutoka katika kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu.

Swala za jamaa zinaswaliwa sehemu tofauti, kuna jamaa ya ndani ya uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na katika uwanja uliopo mkabala na mlango wa Kibla baada ya kuandaliwa kwa ajili hiyo.

Kuhusu majengo ya kutolea huduma yaliyo chini ya Atabatu Abbasiyya ambayo zinaswaliwa swala za jamaa ni kama vile mgahawa (mudhifu) wa nje wa Ataba tukufu, jengo la Shekh Kuleini, jengo la Alqami na mengineyo, sehemu zote swala zinaongozwa na watumishi wa kitengo cha Dini waliopewa jukumu la kufanya tabligh katika siku za ziara ya Arubaini na kuswalisha jamaa, kitengo kiliteua Masayyid na Mashekh watakao swalisha jamaa pamoja na kujibu maswali na kutoa maelekezo kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: