Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu atembelea vituo vya kuingilia mazuwaru na akisifu kikosi cha Abbasi kwa kuimarisha usalama…

Maoni katika picha
Miongoni mwa matembezi anaofanya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Muhammad Ashiqar ni kuangalia huduma zinazo tolewa kwa mazuwaru wa ziara ya Arubaini, na miongoni mwa huduma muhimu ni kuimarisha usalama wao, ametembelea vituo vya kuingilia mazuwaru wanaotokea upande wa Bagdad kuja Karbala, upande ambao kikosi cha wapiganaji cha Abbasi ndio kinacho wajibika kuweka ulinzi.

Sayyid Ashiqar baada ya kukutana na viongozi wanaosimamia kazi hiyo pamoja na wapiganaji, alisifu kazi nzuri inayo fanywa na kikosi cha Abbasi (a.s) ya kuimarisha usalama na kuwahudumia mazuwaru wa Arubaini, akabainisha kua: “Mwaka huu kikosi cha Abbasi kinalinda amani katika vituo vya kuingia Karbala kwa kushirikiana na askari wa kikosi cha Furaat Ausatu pamoja na askari wa mkoa wa Karbala, kama walivyo fanya miaka ya nyuma, na wameonyesha ufanisi wao katika hilo”, akasisitiza kua: “Hakika Atabatu Abbasiyya tukufu imekua mstari wa mbele kusaidia kikosi cha Abbasi (a.s) sambamba na vikosi vingine vya Hashdi”.

Vilevile Mheshimiwa katibu mkuu amekutana na mazuwaru na kusikiliza changamoto wanazo kutana nazo katika matembezi yao, na kawaombea wakamilishe salama ziara yao na warejee salama katika miji yao.

Kumbuka kua kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kina nafasi kubwa katika kuimarisha usalama na kutoa huduma kwa mazuwaru, kimeweka idadi kubwa ya wapiganaji wake katika njia zinazo elekea Karbala, pamoja na kusaidiana na vikundi vingine katika kuwahudumia mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: