Zaidi ya maukibu (2000) zimewahudumia mazuwaru wa Arubaini katika mkoa wa Baabil…

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya cha Ataba mbili tukufu kimetangaza kua: “Idadi ya maukibu zilizo hudumia mazuwaru wa Arubaini katika mkoa wa Baabil mwaka huu na zilizo sajiliwa rasmi imefika (2370), bado kuna makumi ya Husseiniyya na nyumba za watu zilizo toa huduma kuanzia siku ya kwanza bila kusajiliwa”.

Wakafafanua kua: “Maukibu zilisambaa katika njia zote zinazo tumiwa na mazuwaru pamoja na kuwepo kwa wingi zaidi katika njia zinazo tumiwa na mazuwaru wengi, pia kuna mawakibu zingine zimeenda kutoa huduma katika mkoa wa Karbala na katika njia zinazo elekea kwenye mkoa huo”.

Wakabainisha kua: “Mwaka huu misafara ya mazuwaru ilianza kupita mapema kuelekea Karbala, maukibu hazikuishia kutoa huduma peke yake, bali zimetoa ushirikiano mkubwa kwa vyombo vya ulinzi na usalama, baada ya kuisha misafara ya mazuwaru katika mkoa huu, wahudumu wa mawakibu nao wataanza safari ya kuelekea katika mkoa wa Karbala ili wapate utukufu mara mbili, utukufu wa kutoa huduma na utukufu wa kufanya ziara”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: