Kwa macho yao: Mayatima wanapolia na kutokwa machozi pale wanapo kumbuka machozi ya Ruqayyah…

Maoni katika picha
Inapokua kila maukibu Hussein (a.s) inakitu inacho fanya katika njia ya Arubaini, utaona mapinduzi ya milele katika mawakibu Husseiniyya zilizo eneo kila mahala kwa ajili ya kumuhudumia kila anaye kwenda Karbala, mzee, kijana, wanawake kwa watoto, hadi mashahidi ambao picha zao zimepamba barabara walikua wanamkaribisha na kumuhudumia kila anayekuja kwa Hussein (a.s), watoto hawa baada ya kupoteza baba au ndugu kwa ajili ya kulinda taifa, wameamua kuweka maukibu yao katika barabara ya watembea kwa miguu waliyo ipamba kwa bendera za Iraq na mabango yanayo onyesha kilio cha mayatima wanao bubujika machozi, hasa wakikumbuka machozi ya Ruqayyah binti wa bwana wa mashahidi (a.s), hiki ni kielelezo kinacho onyesha athari ya mapinduzi ya Imamu Hussein (a.s) hadi watoto wanapo kumbuka wazazi wao na ndugu zao wanaweka maukibu ya kuwaenzi Hashdi Sha’abi.

Taifa alilolimwagilia Hussein kwa damu yake vizazi na vizazi havina hofu, vina historia ndefu kuanzia tukio la Twafu, tukio la hema, watoto na maji. Kamera ya mradi wa (kwa macho yao) inakuletea picha kutoka katika matembezi ya watu wanaokwenda kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kumbuka kua mradi wa (kwa macho yao) ni mradi wa watangazaji ulio chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, unalenga kuwaletea picha halisi ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), kupitia vyombo vya habari tofauti vya kiaravu na kiajemi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: