Ofisi ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Ayatullahi Sayyid Ali Husseini Sistani imewahusia na kutoa maelekezo kwa mazuwaru wanaokwenda kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), miongoni mwa maelekezo hayo ni: (Waumini walio wezeshwa na Mwenyezi Mungu kuja kufanya ziara hii tukufu yawapasa wafahamu kua Mwenyezi Mungu aliteua mitume na mawasii ili wawe kiigizo chema kwa watu na hoja juu yao waongoke kupitia mafundisho yao na wafuate vitendo vyao.
Na Mwenyezi Mungu amehimiza kuwatembelea ili kudumisha kumbukumbu zao na uwe ni ukumbusho wa watu kwa Mwenyezi Mungu mtukufu na mafundisho yake na hukumu zake, hakika wao walikua mfano mkubwa katika kumtii Mwenyezi Mungu na kupigania njia yake na kujitolea kwa ajili ya Dini yake tukufu).
Akahitimisha usia huo kwa kuomba dua ifuatayo: “Tuna muomba Mwenyezi Mungu mtukufu aongeze utukufu na heshima ya Mtume Mustwafa (s.a.w.w) na Ahlulbait wake watakatifu (a.s) hapa Duniani na Akhera, kutokana na namna walivyo jitolea katika njia yake na wakapigana jihadi kwa ajili ya kuwaokoa waja wake, na awaongezee amani kama alivyo watakia amani walio kua kabla yao hususan Ibrahim na Aali Ibrahim, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awabariki mazuwaru wa Hussein (a.s) katika ziara yao na awakubalie kama anavyo wakubalia waja wema, hadi wawe mfano mwema katika matembezi haya ya ziara na katika maisha yao yote, na awalipe kwa utukufu wa Ahlulbait (a.s) kutokana na kuwa kwao wafuasi wema wanaofuata mwenendo wao na kufundisha ujumbe wao, tunategemea awaite (a.s) katika siku ambayo kila mtu ataitwa na Imamu wake, na watakaopata shahada katika njia hii wafufuliwe pamoja na Hussein (a.s) na maswahaba wake waliojitolea nafsi zao kwa ajili ya mapenzi yao kwake, hakika yeye ni mwingi wa kusikia mwingi wa kujibu).