Kwa ushiriki wa mubalighina wa kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu tena mwaka wa sita mfululizo, zimeswaliwa swala za jamaa za Dhuhuraini kubwa na ndefu sana kwa wakati mmoja, wamesimama kuswali maelfu ya watu wanaume kwa wanawake nyuma ya maimamu wapatao (750) kuanzia katika nguzo namba (96) kama ukiwa unaelekea Karbala tukufu, swala hiyo ya jamaa imeongozwa na mamia ya wanafunzi wa hauza ya Najafu ilikua na urefu wa kilo meta arubaini katika njia ya (yaa Hussein) katika eneo la baina ya Najafu na Karbala, mazuwaru wameonyesha msimamo wa Imamu Hussein (a.s) katika siku ya Ashura, hakuogopa mikuki wala mishale kuelekea kwa Mola wake Mlezi.
Swala ya jamaa ya pamoja mwaka huu imeanzia katika nguzo namba (96) sehemu ilipo maukibu ya Atabatu Abbasiyya tukufu na imeendelea hadi kwenye nguzo namba (950), zikiwemo swala za jamaa za wanawake kuanzia nguzo ya (679 hadi nguzo ya (689) katika maukibu ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, na katika nguzo ya (208) sehemu kilipo kituo cha mradi wa tabligh, jamaa hii iliongozwa na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Ashkuri, na katika mgahawa (mudhifu) wa Atabatu Abbasiyya iliongozwa na Sayyid Adnani Mussawi.
Vyombo vingi vya habari vimeripoti tukio hili na kuonyesha picha halisi duniani, ili watu wote waone kuwa sisi ni wamoja, na hatumnyenyekei yeyote ispokua Mwenyezi Mungu Mlezi wa walimwengu, na njia ya Hussein (a.s) ni njia inayo unganisha watu, na watu wanaopita katika njia yake hawako tayali kuacha kufanya haki hata kama itawagharimu, pamoja na haraka kubwa waliyo nayo ya kufika Karbala, haijawazuia kutekeleza faradhi waliyo faradhishiwa na Mwenyezi Mungu kwa wakati na unyenyekevu wa hali ya juu.