Atabatu Abbasiyya tukufu yazindua mradi wa utangazaji wa kimataifa kwa ajili ya kuitambulisha ziara ya Arubaini na kuwavutia mazuwaru wa kiarabu na kiajemi…

Maoni katika picha
Makumi ya mahojiano yaliyo rekodiwa kwenye video yametafsiriwa katika lugha mbalimbali, na idadi kadhaa ya filamu zinaandaliwa katika mradi huu wa utangazaji unao tekelezwa na Atabatu Abbasiyya tukufu na kuzilenga nchi za Magharibi.

Mkuu wa kituo cha utamaduni na habari za kimataifa Alkafeel cha Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Jasaam Muhammad Saidiy ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kua: “Hakika mradi huu unahusisha mahojiano ya makumi ya viongozi -wa Dini, Utamaduni na Siasa katika nchi zao- wasiokua waarabu na waarabu miongoni mwa mazuwaru wa Arubaini, uradi unalenga kuitambulisha ziara ya Arubaini na kuonyesha picha halisi ya Iraq kwa ajili ya kuwavutia mazuwaru wa kigeni na wakiarabu, na kuonyesha picha nzuri kimataifa baada ya kuchafuliwa kwa kiasi kikubwa na vyombo vya habari”.

Kuhusu jina la mradi huu amesema kua: “Mradi huu tumeuita (ujumbe wa Arubaini) kwa sababu msimu huu umechukua karne (13) na nusu za kusambaza ujumbe wa amani na mapenzi katika kulea vizazi na vizazi vya wairaq vinavyo ishi katika mazingira ya kujitolea na kusubiri na kufanya kila zuri bila mipaka, na ikawa miongoni mwa matunda yake ni kupatikana kizazi kilicho washinda magaidi wa Daesh kwa muda mdogo zaidi (mara kumi) chini ya muda uliotajwa na viongozi wa kisiasa wa Marekani baada ya kuanza tatizo la Daesh, yapasa masomo ya tukio hili yasambae kwa kila anayeshiriki kutoka nchi zote Duniani, jambo hilo ndio linaloonekana katika mahojiano ambayo hata wasio kua waislamu wamekiri kunufaika na ujumbe wa Arubaini katika kumjenga mwanaadamu”.

Kuhusu usambazaji wa matukio ya mradi huu Saidiy amesema kua: “Tumefungua mtandao na ukurasa wa youtube kwa jina hilo hilo, na tumetafsiri filamu na majadiliano kupitia Darul Kafeel kitengo cha tarjama kilicho chini ya kituo hiki, pia tumetafsiri kutoka lugha zingine za (kiengereza, kifaransa, kituruki na kiurdu) na kuleta lugha ya kiarabu ili ziwe rafiki kwa wazungumzaji wa kiarabu”.

Kumbuka kua kituo cha utamaduni na habari za kimataifa Alkafeel kinaharakati tofauti na miradi mbalimbali, kilianzishwa kwa ajili ya kufikisha fikra za Ahlulbait (a.s) kupitia lugha za kimataifa ili kila mtu apate ujumbe kupitia lugha yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: