Miongoni mwa maswali yaliyo elekezwa katika ofisi ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani kuhusu baadhi ya mambo yanayo husiana na usafi katika ziara ya Arubaini tukufu, tunakuletea moja ya maswali hayo.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.
Asalaamu alaikum wa rahmatullahi wa barakaatuhu..
Kutokana na kukaribia ziara tukufu ya Arubaini, tunapenda kuwauliza kuhusiana na usafi katika utekelezaji wa ziara, baada ya idadi ya mazuwaru kufikia mamilioni na ugumu wa kudhibiti mambo, na mapungufu yanaonekana wazi.. je kuna nasaha yeyote unayo weza kutupa sisi watu wa mawakibu na mazuwaru kuhusu usafi na kuweka utaratibu mzuri wa kuhudumia mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s)?
Jibu la ofisi lilikua kama ifuatavyo:
Kila mtu anatakiwa kulinda usafi, hakika usafi unatokana na imani –kama ilivyo pokewa katika hadithi tukufu-, pia wanatakiwa kusaidiana katika kupangilia ziara hii katika hali nzuri ili kuhakikisha mazingira mazuri na usalama kwa mazuwaru, uzuri ulioje kwa zaairu utakapo kua muonekano bora wa usafi na mpangilio, utokanao na adabu nzuri ya jamii ya mazuwaru na mwenendo bora, tunamuomba Mwenyezi Mungu awawezeshe mazuwaru wote kufanya ziara kwa kufuata adabu zake na awakubalie idaba zao hakika yeye ni mkuu wa kuwezesha..