Wanawake wana nafasi sawa na wanaume katika kuwahudumia mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s)…

Maoni katika picha
Watu wema hawajulikani ispokua kwa vitendo vyao, inapokua bendera ya utukufu ndio anuani ya njia, utakuta katika ya halaiki ya Husseiniyya kuna wazee, vijana, wanawake na watoto, wote wanashindana kunyanyua bendera ya bwana wa mashahidi (a.s).

Kama ulivyo utukufu wa wanaume katika mawakibu za Husseiniyya, hivyo hivyo wanawake nao wanautukufu katika kuwahudumia mazuwaru wa Arubaini, kuna wanawake wanao toa huduma katika mawakibu za Karbala huku wakisema (uwe mbali nasi udhalili), wanaomboleza na kumpa pole mbora wa wanawake kwa kuuliwa mtoto wake, pamoja na shujaa mtetezi kwa kuuliwa ndugu zake na kutekwa familia yake, Bibi Fatuma Zaharaa na bibi Zainabu (a.s).

Miongoni mwao kuna wanaoshiriki kuwahudumia mazuwaru, wanasaidiana na watoto wao kutoa huduma kwa mazuwaru baada ya kufungua milango ya nyumba zao na kuzifanya ni maukibu za Hussein, na kuna wanao shiriki kazi za uuguzi katika vituo vya afya, na wengine wanashiriki katika hema za kusahihisha usomaji wa surat Fat-ha na kufundisha usomaji sahihi, huku wengine wakiunda vikundi vya utangazaji na kurusha picha halisi ya matembezi ya Husseiniyya kwa walimwengu, pia kuna wanaosimama karibu na mawakibu pamoja na vituo vya kupumzika kwa ajili ya kuwakaribisha mazuwaru kwenda kulala katika nyumba zao na baada ya kumpata zaairu katika nyumba yake anakesha akimuhudumia hadi saa atakayo ondoka.

Wanawake wamekua wakitoa huduma mbalimbali na wanauonyesha ulimwengu kua mapinduzi ya Hussein ni mapinduzi dhidi ya dhulma na utwaghuti, hakika Hussein amebeba ujumbe wa amani unao waneemesha walimwengu wote, pamoja na huduma zote hizo kuna mama wa kiiraq amesimama mlangoni akiwa amejaa vumbi, anahimiza mabinti zake kutengeneza mikate na anawakaribisha mazuwaru kwa kuwaambia (karibuni mazuwaru wa Abu Ali), hajaacha kufanya hivyo hadi zaairu wa mwisho apite na kula katika mikate yake.

Mwenyezi Mungu awalipe watumishi wa Hussein na awaangazie njia yao na kuwafanya kua kiigizo chema kwa wanawake wote wa duniani vizazi na vizazi, na awape mwisho mwema na awafufue pamoja na mbora wa wanawake bibi Fatuma (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: