Madrasa ya Husseiniyya inasifika kwa utowaji wa elimu bora kwa sababu ndio njia ya kuongoza watu wote, atabatu Abbasiyya tukufu imejitahidi kudumisha harakati zake kila mwaka kwa ajili ya kunufaika na ziara za milionea, ikiwemo ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), kwa ajili ya kuwaelimisha watu kuhusu mambo ya utamaduni, Dini na mengineyo, chini ya mwenendo wa Imamu Hussein (a.s) kupitia vitabu na machapisho yake.
Maonyesho ya vitabu chini ya kitengo cha habari na utamaduni na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu pamoja na kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, ambayo yanafanyika karibu na uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), yamepata mwitikio mkubwa katika ziara hii, mazuwaru wanamiminika kuangalia vitabu na machapisho mbalimbali yenye mafundisho ya kidini na kibinaadamu, na yanayo endana na mahitaji ya rika tofauti katika jamii na watu watabaka mbalimbali, maonyesho haya huanza saa mbili asubuhi na huendelea hadi usiku mwingi.
Mwitikio huo haujahusisha raia wa Iraq peke yao, bali watu kutoka nchi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Iran, Sirya na Lebanon, asilimia kubwa ya watu wanao kuja katika maonyesho haya wanaangalia zaidi vitabu vya Dini, Turathi na maarifa mbalimbali, pamoja na vitabu vya maendeleo ya wanaadamu na fani mbalimbali.
Wadau wa maonyesho haya wameisifu Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuweka machapisho yanayo fundisha elimu na utamaduni wa Ahlulbait (a.s) katikati ya mafuriko ya wafuasi na wapenzi wao wanaokuja Karbala kutoka kila mahala.