Hali ya Karbala sasa hivi (kwa picha): watu wamefurika juu ya uwanja wake…

Maoni katika picha
Mwaka baada ya mwaka, watu wanasahau marehemu wao, na huzimika moto wa huzuni zao mbele ya msiba mkubwa, ni mpenzi mmoja tu ambaye moto wa huzuni unaendelea kuwaka katika moyo wa kila muislamu na kizazi baada ya kizazi, madamu Mwenyezi Mungu mtukufu amewajibisha kumpenda Mtume Muhammad (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake (a.s) ili awalipe thawabu kwa hilo, basi wajibu huo unatekelezeka kwa kuomboleza msiba wa Imamu Hussein kila mwaka.

Mwanzoni mwa siku ya kukumbuka arubaini ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) mji wa Karbala umekua kama bahari iliyo furika watu, makundi kwa makundi ya watu wanaendelea kumiminika katika mji wa Karbala kupitia kila njia inayo ingia kwenye mji huu huku wanasema: Yaa Hussein yaa Hussein.. sauti zao zinapaa hadi mbinguni.

Kamera ya Alkafeel ilikua pamoja na makundi ya mazuwaru katika usiku wa Arubaini, na inakuletea baadhi ya picha zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: