vituo vya kuongoza walio potea, wazee na watoto…

Maoni katika picha
Miongoni mwa huduma zinazo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mazuwaru wa Arubaini, ni uwekaji wa vituo vya kuelekeza walio potea, wazee na watoto katika barabara zinazo elekea Karbala pamoja na ndani ya mji wa Karbala, vituo hivyo vinatoa huduma mbalimbali za kibinaadamu, miongoni mwa huduma hizo ni:

  • - Kuandika taarifa za mtoto au mzee kwenye kitambulisho maalumu ambacho kinabebeka kwa urahisi, kinaandikwa jina la muhusika na maelezo yatakayo saidia kumtambua kama akipotea.
  • - Vituo hivyo vina namba ya kupiga simu bure kupitia mtandao wa (Asia seel) kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano baina ya vituo pamoja na kituo kikuu (kituo cha Alkafeel kwa waliopotea cha Atabatu Abbasiyya tukufu).
  • - Kuna vipaza sauti vinavyo tumika kutangaza aliye potea au kilicho potezwa hiyo ikiwa kama hatua ya kwanza.
  • - Kuna magari ya kubeba walio potea au vilivyo potezwa hadi karibu na mahala walipo wa husika wake.

Kitengo cha magodauni kimechapisha karibu vitambulisho milioni moja kwa ajili ya shughuli hii, sekta hii inasimamiwa na watumishi wa kitengo cha magodauni pamoja na watu wanaojitolea wenye uzowefu wa kazi hizi, vituo hivi katika ziara iliyo pita vilifanikiwa kuwakutanisha maelfu ya walio potea na watu wao mubashara au kupitia vituo vya walio potea na vilivyo potezwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: