Bendera zimekuja kutoka nchi mbalimbali na kukutana katika anga la Karbala…

Maoni katika picha
Kama makundi ya nyuki, wanakuja wameinua vichwa vyao juu, wote wakitaja jina la Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi na watu wengine wa Ahlulbait (a.s), bendera zimekuja kutoka nchi za nje na zingine kutoka katika miji ya Iraq, zote zinakutana katika anga la Karbala, kama vile ujumbe kwa matwaghuti walio pambana na misingi ya Imamu Hussein (a.s) na wakasimama kuzuia mazuwaru wake. Hizi hapa bendera za Abu Abdillahi Hussein zinapepea katika anga la uhuru toka karne za nyuma hadi leo, zinatangaza ushindi wa Mtume Muhammad na watu wa nyumbani kwake (a.s), zinapamba barabara na kutuma ujumbe wa furaha katika nyoyo za wapenzi wao kutokana na ushindi dhidi ya maadui wao.

Bendera zimebebwa na mikono ya watu tofauti, mikono ya wazee, vijana, watoto na wanawake, kama vile wanamuambia jabali wa subira bibi Zainabu (a.s): sisi wote leo ni panga kali za Hussein na hizi ni bendera za Abulfadhil ewe bibi wa subira zimebebwa na mikono ya wapenzi wake katika kila zama, amani iwe juu yako na juu ya watu wa nyumbani kwako ewe mtukufu wangu, amefaulu mwenye kubeba bendera zenu na kuzipeperusha angani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: