Inatokea hivi sasa: Mafuriko ya watu walio ungana dhamira zao na kuchanganyika sauti zao wanamiminika katika kaburi la Hussein (a.s)…

Maoni katika picha
Maombolezo makubwa zaidi yamefika ukingoni mwake, mamilioni ya waumini wamekuja katika mji wa Karbala kuzuru kaburi la bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), wakiwa wamejaa mapenzi kwa watukufu hawa walio lala katika ardhi hii takatifu, watu hawa ni sawa na mwili mmoja wenye roho moja wanakuja kwa Imamu mmoja, kwa ufupi tunaweza kusema kua wameunganishwa na Imamu, hakuna mtu yeyote ispokua wapo walio muwakilisha katika ardhi ya Karbala ya Hussein (a.s), watu wanao ingia na kutoka katika mji huo wanaonyesha imani kubwa na mapenzi ya hali ya juu kabisa kwa Ahlulbait (a.s) na wote wamekwenda kuhuisha utiifu wao kwa Abul-Ahraar (a.s).

Hawa hapa wanamiminika katika kaburi lake wakiwa mtu mmoja mmoja na vikundi (mawakibu) kwa vikundi, umoja wao hauonyeshi tofauti, Hussein ndio jambo lao la kwanza na la mwisho, na kudumisha ziara ya Arubaini ndio lengo lao la kudumu, kama anavyo ona kila mwenye macho kinacho tokea katika ardhi ya Karbala, mamilioni ya watu wanao miminika Karbala wote wanaomba Mwenyezi Mungu aidumishe ziara hii vizazi na vizazi.

Kwa upande mwingine, Atabatu Abbasiyya tukufu imetumia uwezo wake wote kuhakikisha mazuwaru wanatekeleza ibada zao kwa amani na utulivu, ziara hii ilianza mapema na siku ya leo ndio kilele chake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: