Kitengo cha maadhimisho na mawakibu: Zaidi ya maukibu (29,000) za kutoa huduma na kuomboleza zimeshiriki katika ziara ya Arubaini zikiwemo (227) kutoka nchi za kiarabu na kiajemi…

Maoni katika picha
Rais wa kitengo cha maadhimisho, mawakibu na vikundi vya Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya bwana Riraadh Ni’mah Salmaan ametangaza kua: “Jumla ya mawakibu zilizo shiriki kutoa huduma na kuomboleza katika ziara ya Arubaini mwaka huu zimefika (29,043), huku zingine zikitoka miji ya mbali kabisa hapa Iraq na maukibu (227) kutoka katika nchi za kiarabu na kiajemi”.

Akaongeza jua: “Baadhi ya maukibu hizo zilikua na pande mbili, utowaji wa huduma na uombolezaji (matam na zanjiil) na zingine zilikua na upande mmoja tu, mgawanyo wa maukibu hizo kwa mujibu wa mikoa ya Iraq upo kama ufuatavyo: (Dhiqaar maukibu 3570) – (Muthanna maukibu 1103) – (Waasit maukibu 3150) – (Basra maukibu 3563) – (Misaan maukibu 701) – (Bagdad maukibu 5383) – (Swalahu Dini maukibu 252) – (Diyala maukibu 677) – (Karkuuk maukibu 164) – (Nainawa maukibu 42) – (Najafu Ashrafu maukibu 554) – (Diwaniyya maukibu 2214) – (Baabil maukibu 2370) – (Karbala tukufu maukibu 4550)”.

Akabainisha kua: “Maukibu zilizo toka katika nchi za kigeni (za kiarabu na kiajemi) ni (227) kutoka katika nchi (24) ambazo ni: (Oman, Bahrain, Qatar, Kuwait, Saudia, Yemen na Lebanon) nchi za kiarabu, na nchi za kiajemi ni: (Adharbaijani, Iran, Afghanistani, Swiden, India, Marekani, Indonesia, Pakistani, Ubelgiji, Tailend, Uturuki, Tanzania, Uingereza, Kanada, Holandi, Ufaransa na Kenya)”.

Akaendelea kusema kua: “Mawakibu za kutoa huduma zilianza kazi tangu siku za mwanzo walipo anza kuwasili mazuwaru, na baadhi yake zitaendelea kuwepo hata baada ya kumaliza ziara na zimesajiliwa rasmi na kukamilisha taratibu zote za kiusalama, kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao na kubainisha taratibu zao na mahala walipo”.

Akamaliza kwa kusema: “Kuna maukibu nyingi ambazo zimetoa huduma bila kusajiliwa pamoja na nyumba za watu walio kuwa wanatoa kila aina ya huduma kwa mazuwaru bila kuwa na usajili wowote, huduma zinazo tolewa na maukibu hizo ni chakula, vinywaji, malazi na huduma za kitabibu pamoja na kuratibu watembeaji, pia kuna huduma zingine za kiufundi, kama vile kutendeneza mikokoteni ya kubeba watoto na wazee, kufua ngua na kuzinyoosha, pamoja na tiba za asili, wametumia uwezo wao wote katika kutoa huduma tena wanashindana kuhudumia watu kwa ajili ya kutafuta thawabu”.

Tunapenda kuwajulisha kua ziara ya Arubaini inaendelea kupata ongezeko kubwa la mawakibu na vikundi vya kutoa huduma sambamba na ongezeko kubwa la mazuwaru mwaka baada ya mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: