Vyombo vya habari (240) vimeshiriki kurusha ziara ya Arubaini…

Maoni katika picha
Kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kua jumla ya vyombo vya habari (240) vya kitaifa na kimataifa vya rulinga magazeti na mitandao ya kijamii, vimeshiriki kurusha matangazo ya ziara ya Arubaini, vikiwakilishwa na waandishi wa habari (1100) miongoni mwao (250) kutoka nchi za kigeni, pamoja na wapigapicha zaidi ya (10,000) wengi wao wakiwa chini ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, walitapakaa katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na eneo la katikati ya haram mbili tukufu, chini ya utaratibu maalumu ulio wekwa unao saidia kuonyesha picha halisi ya ziara ya Arubaini, pamoja na kuwapa kila walicho hitaji kwa ajili ya kutekeleza wajibu wao.

Hayo yamesemwa na makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Aqiil Abdulhussein Yasiriy, akaongeza kua: “Ziara ya Arubaini ya mwaka huu imeripotiwa na vyombo vingi vya habari kutoka ndani na nje ya Iraq, vikiwemo vyombo ambavyo vimeshiriki kwa mara ya kwanza kutangaza tukio hili muhimu, asilimia kubwa vilianza kazi mara tu baada ya mazuwaru kuanza kuwasili katika mkoa wa Karbala, na wamefanikiwa kurusha picha halisi ya ziara hii”.

Akabainisha kua: “Kwa ajili ya kupangilia vizuri kazi ya utangazaji wa ziara ya Arubaini kwa namna ambayo inawawezesha kurusha picha halisi ya ziara hii tukufu, bila kikwazo chochote, kitengo kiliweka utaratibu maalumu, kuanzia upokeaji wa maombi kutoka kwa chombo cha habari kilicho taka kurusha matukio ya ziara hii, kisha chombo hicho kilisajiliwa rasmi katika orodha maalumu ya vyombo vya habari na kutengenezewa kitambulisho (baji) na kopi ya kitambulisho hicho kupewa Atabatu Husseiniyya tukufu na viongozi wa eneo la uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, ili kurahisisha utendaji baina yao kwa kufuata utaratibu na njia tulizo kubaliana”.

Akasema: “Kupitia kituo cha uandaaji wa vipindi Alkafeel chini ya kitengo chetu, tuliandaa masafa maalumu kwa ajili ya kurusha bure matukio ya ziara ya Arubaini yaliyo kua na ubora mkubwa na kuwezesha vyombo vya hapari kupokea matangazo kutoka katika masafa hiyo, matangazo hayo yalionyesha haram tukufu ya Abu Abdillahi Hussein na haram ya ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) zaidi ya upande mmoja, pamoja na eneo la katikati ya haram mbili tukufu sambamba na kufuatilia matembezi ya mazuwaru kuanzia miji ya mbali kabisa kusini mwa Iraq hadi Karbala”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: