Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara ya maji bwana Haidari Hanuun amesema kua: “Kugawa maji kwa mazuwaru na mawakibu ni jambo muhimu sana katika ziara ya Arubaini, uhitaji wa maji umeendelea kuongezeka ukizingatia mwaka huu ziara imesadifu kipindi cha choto kali, ugawaji wa maji safi ya baridi umefikia lita milioni moja kwa siku hadi wakati wa kuandika taarifa hii, kwa utaratibu ufuatao:
- - Kusambaza maji kwa kutumia magari maalumu ya maji katika mawakibu kipindi chote cha ziara, katika barabara za Bagdad, Hilla, Najafu hadi katika majengo ya kutolea huduma ambayo yapo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na sehemu za barabara ya Maitham Tammaar ambayo inaidadi kubwa ya maukibu.
- - Kusambaza maji katika vituo vya Atabatu Abbasiyya na maukibu zilizo karibu na vituo hivyo.
- - Kusambaza maji ndani ya uwanja wa hara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kujaza maji katika madeli yaliyopo ndani ya eneo hilo tukufu na katika sarbabu (handaki) sehemu za ndani na nje, madeli hayo yalikua yanajazwa maji muda wote saa (24).
- - Kusambaza maji katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu na katika barabara na njia za karibu na eneo hilo, zikiwemo sehemu zote za ukaguzi na kila mahala palipo na deli la maji, kazi hiyo imefanywa na magari maalumu yaliyo pangiwa jukumu hilo.
- - Kusambaza maji katika nyumba zilizo karibu na haram tukufu, ambapo walipewa maji moja kwa moja au kupitia wakazi wa nyumba hizo.
- - Kusambaza maji katika maeneo yaliyo andaliwa na Atabatu Abbasiyya kwa ajili ya kulala mazuwaru katika majengo ya shule na Husseiniyya.
- - Kuweka tenki za maji zenye ujazo wa (lita 1000) katika maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu, kama vile barabara ya Jamhuriyya. Pia kulikua na aina nyingine ya kugawa maji katika grasi maalumu, ugawaji huo ulitumika kwa madereva na watu wanao simamia usafiri katika vituo vifuatavyo:
- - Kituo cha kubeba mazuwaru cha Baabil Karbala.
- - Kituo cha kubeba mazuwaru cha Bagdad Karbala.
- - Kuweka vituo vya kugawa grasi za maji kwa mazuwaru na mawakibu”.
Akabainisha kua: “Tuliandaa magari rasmi kwa kazi hiyo, na watumishi wa idara hii wamefanya kazi mfululizo kutokana na wingi wa watu walio kua wanaongezeka kila muda katika njia zote, kwahiyo kulikua na zamu mbili kila siku, zamu ya kuingia asubuhi na zamu ya kuingia jioni”.