Makumbusho ya Alkafeel ya vifaa na nakala kale ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imetembelewa na idadi kubwa ya mazuwaru katika kipindi cha ziara ya Arubaini, wameangalia vitu vilivyopo ndani ya makumbusho na wameonyesha kufurahishwa navyo sana.
Katika kipindi chote cha ziara ya Arubaini makumbusho ilikua inafurika watu kutoka nchi tofauti duniani, wameonyesha kufurahishwa sana na kazi nzuri inayo fanywa na makumbusho hii ya kuhifadhi turathi za kiislamu, imetembelewa na watu kutoka katika nchi za kiarabu na kiajemi, maka vile: Uingereza, Ufaransa, Marekani, China, Uturuki, Adharbaijani, Iran, Pakistani, India, Gini, Moroko, Aljeria, Baharain, Saudia, Kuweit, Oman na Sirya. Mazuwaru walivutiwa sana na kiriba cha Abulfadhil Abbasi (a.s) ambacho kinaonekana kua kinafanana zaidi na kiriba halisi alicho tumia mwezi wa familia Abulfadhil Abbasi (a.s) katika vita ya Twafu na kumpa heshima kubwa ya kuwapa maji wafuasi wa Imamu Hussein na Ahlulbait (a.s).
Kumbuka kua makumbusho ya Alkafeel ya vifaa na nakala kale ndio makumbusho ya kwanza kufunguliwa katika Ataba za Iraq, na ilifunguliwa mwaka (20009m) katika kumbukumbu ya kuzaliwa bibi Zainabu (a.s), makumbusho hii inavifaa vingi vya kihistoria ambavyo baadhi yake historia yake inarudi katika mamia ya miaka (karne na karne).