Baada ya kumaliza ziara ya Arubainiyya: Kitengo cha utumishi cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza kusafisha mji mtukufu wa Karbala…

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya Juma Tano (21 Safar 1440h) sawa na (31 Novemba 2018m) wameanza kazi ya kusafisha mji mtukufu wa Karbala, baada ya kuisha ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) na kuondoka mazuwaru katika mji.

Kuhusu shughuli hiyo ya usafi makamo rais wa kitengo cha utumishi Ustadh Alaa Abdulhussein ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Asubuhi ya Juma Tano (21 Safar 1440h) imeanza kazi ya kuusafisha mji mtukufu wa Karbala baada ya kumaliza ziara ya Arubainiyya, kazi hiyo imeanzia katika ofisi za Tarbiya kuelekea katika mji mkongwe na maeneo ya karibu na haram mbili tukufu, kisha wakaelekea pande tatu zilizo tumiwa na mazuwaru wengi kuingia Karbala, ambazo ni upande wa mlango wa Bagdad na upande wa mlango wa Towareji na upande wa Najafu, pande zote hizo zilikua zimewekwa mapipa ya kutupia taka na mifuko kila mahala, kiwango cha taka zilizo kusanywa katika sehemu hizo kimefika tani (10)”.

Akaoneza kua: “Kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi mwaka huu tumeongeza eneo la kufanya usafi, tutafika hadi katika kitongoji cha mto wa Hindiyya na kitongoji cha mto wa Bobiyaat, tumekubaliana na idara ya mazingira ya mkoa kuhusu kuanzisha utaratibu wa kuondoa uchafu katika mito kwa kutumia mitambo maalumu”.

Akasema: “Tunaendelea kufanya usafi hadi katika mji wa Haidariyya, tunafanya kazi saa (24) tuna zamu mbili kwa siku kila zamu inasaa (12)”.

Kumbuka kua kitengo cha utumishi kimefanya kila kiwezalo katika kuwahudumia mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) wakati wa ziara ya Arubainiyya, wakisaidiwa na wafanyakazi wa kujitolea waliokuja Karbala kutoka mikoa tofauti ya Iraq ambao idadi yao ilikua zaidi ya watu (3000).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: