Kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu akutana na wawakilishi wa kundi la madaktari walioshiriki kutoa huduma katika ziara ya Arubaini mwaka huu (1440h)…

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amekutana na wawakilishi wa madaktari walio shiriki kutoa huduma kwenye mahema ya huduma za afya yaliyo fungwa katika ziara ya Arubaini ya mwaka huu 1440h, Mheshimiwa aliwashukuru sana kutokana na huduma walizo toa kwa mazuwaru.

Katika kikao hicho walijadili mambo mengi, miongoni mwa mambo hayo ni:

  • 1- Umuhimu wa kuwepo kwa kituo cha afya cha dharura kitakacho kua cha kudumu, kwa ajili ya kupokea wagonjwa wa dharura na kuwatibu kwa kufuata misingi ya udaktari.
  • 2- Umuhimu wa kuunda kamati ya pamoja baina ya madaktari wageni na viongozi kutoka katika Ataba tukufu kwa ajili ya kurahisisha utatuaji wa baadhi ya changamoto na kuboresha huduma.
  • 3- Kuwepo na kamati au idara ya wataalamu wa mambo ya tiba (madaktari) itakayo fanya tathmini ya mazingira ya baadae na kuangalia kinga za maradhi tarajiwa wakati wote.
  • 4- Umuhimu wa kuwa na mkakati wa kupambana na majanga utakao andaliwa na wataalamu wa elimu ya majanga.

Mjumbe wa kamati ya uongozi wa Munadhamat Imamiyya Twibiyya Al-Aalamiyya Dokta Qassim Jafari akazungumzia kuhusu shughuli za kimatibabu zilizo tolewa na kituo cha mlango wa Bagdad (IMI), ambacho kilibadilishwa na kua kituo cha dharura kwa kua kilikua na vifaa tiba vyote muhimu na jopo la madaktari lililo kamilika.

Kilikua kinatoa huduma za hatua tatu, hatua ya kwanza ya upimaji na kubaini tatizo, kisha kutoa dawa za kutibu tatizo hilo, mgonjwa anaweza kuhitaji kwenda hatua ya pili, ya kufanyiwa vipimo vikubwa, na anaweza kupelekwa hatua ya tatu kabla ya kumpeleka katika hospitali (kubwa) ya Husseini.

Mkuu wa jopo la madaktari kutoka Pakistani Dokta Ali Asadi akasema kua, kikundi chake kimekuwa kikitowa huduma za matibabu kwa muda wa miaka mitano, mwanzoni walikua wanafanya kazi katika hospitali ya Maitham Tammaar (r.a), miaka mitatu ya nyuma wameanza kufanya kazi katika uwanja wa Aljuud mkabala na Mlango wa Kibla wa Abulfadhil (a.s).

Mwisho wa kikao hicho Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi aliwaomba wawasilishe mapendekezo yao rasmi ili Atabatu Abbasiyya tukufu iangaliye yale itakayo weza kuyatekeleza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: