Muhimu.. Sayyid Ahmad Swafi: Idadi ya mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) mwaka huu 1440h imefika (15,322,949)…

Maoni katika picha
Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi ametaja idadi ya mazuwaru walio ingia katika mji mtukufu wa Karbala mwaka huu kwa ajili ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), katika khutuba ya Ijumaa ya leo (23 Safar 1440h) sawa na (2 Novemba 2018m) katika uwanja wa haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s).

Amebainisha kua mazuwaru walio ingia katika mji mtukufu wa Karbala kutoka ndani na nje ya Iraq kuanzia mwezi (7 Safar hadi mwezi 20 saa 6 usiku) imefika (15,322,949) kupitia barabara tano ambazo ni: (barabara ya Bagdad, barabara ya Baabil, barabara ya Najafu, barabara ya Husseiniyya, na barabara ya Huru iliyo ongezwa mwaka huu).

Akaongeza kua: “Tumetumia namba katika kuhesabu watu, tulifunga kamera zinazo hesabu watu wanao ingia tu pamoja na magari, na tulikua tunaweka makadirio ya kiwango cha chini kinacho kubalika kiakili sambamba na idadi ya gari zinazo ingia katika mji mtukufu wa Karbala”.

Akamaliza kwa kusema kua: “Idadi ya mawakibu na vikundi vya kutoa huduma imefika (10,714) kutoka katika nchi (25) katika hizo maukibu (225) kutoka nje ya Iraq”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: