Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu wataja idadi ya mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) kwa mujibu wa mtambo wa kielektronik wa kuhesabu watu…

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetaja idadi ya mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) kwa mujibu wa mtambo wa kielektronik wa kuhesabu watu katika mji mtukufu wa Karbala, na hii ndio nakala ya tamko hilo:

Asalamu alaika yaa Abulfadhil Abbasi.. tunatuma rambirambi zetu kwa Imamu wa zama zetu Hujjat bun Hassan (a.s) na Maraajii watukufu, na ulimwengu wote wa kiislamu, hususan Iraq nchi ya Mitume, Mawasii na Mawalii, kutokana na kumbukumbu ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), tunamuomba Mwenyezi Mungu azilinde nchi za kiislamu na kila baya, na awarudishe mazuwaru wa Abu Abdillahi Hussein (a.s) katika miji yao wakiwa salama na wenye kunufaika kwa kukubaliwa ibada zao, thawabu za ziara ziwafikie pia mashahidi watukufu kwani ndugu zao hawakuwasahau katika dua, kutokana na utukufu wa ndugu zao wapiganaji walio itikia wito wa fatwa ya kujilinda ulio tolewa na Marjaa Dini mkuu na ukapatikana ushindi dhidi ya magaidi wa Daesh, na kupata neema hii, tukafanikiwa kuokoa taifa letu na mataifa ya jirani na hatari ya maangamizi.

Kama kawaida yetu kwa zaidi ya karne 13, mji mtukufu wa Karbala umekua ukipata mazuwaru wa bwana wa mashahidi Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), katika ziara ya Arubaini ya mwaka huu 1440h, ilikua fahari kubwa kwa Ataba tukufu kutoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru, ikiwemo huduma ya kuhesabu mazuwaru wanaoingia katika mji mtukufu wa Karbala kupitia barabara kuu kwa kutumia mtambo wa kielektronik, kazi iliyo simamiwa na idara ya mawasiliano ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mwaka wa tatu mfululizo, taarifa zilizo hakikiwa kuhusu idadi ya mazuwaru walio ingia katika mji mtukufu wa Karbala kwa mujibu wa kituo cha Alkafeel cha elimu na uchunguzi wa takwimu.

Idadi ya mazuwaru waliosajiliwa katika mtambo wa kielktronik uliowekwa katika barabara (pande) kuu tano za kuingia Karbala, ambazo ni: (Bagdad – Karbala, Baabil – Karbala, Najafu – Karbala, Husseiniyya - Karbala, Huru – Karbala) ni mazuwaru (15,322,949), usajili huo ulianza mwezi (7 Safar) hadi mwezi (20 Safar) saa sita usiku mwaka 1440h. fahamu kua idadi ya mazuwaru wa mwaka jana 1439h, walikua mazuwaru (13,874,818) na mwaka zuzi 1438h, walikua (11,210,367), tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awakubalie wote, na atuwezeshe katika yale anayo yapenda na kuyaridhia, hakika yeye ni mwingi wa kusikia na mwingi wa kujibu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: