Kitengo cha usimamizi wa kihandisi chapiga hatua katika ujenzi wa bweni la chuo kikuu cha Al-Ameed…

Maoni katika picha
Kitengo cha usimamizi wa kihandisi kimepiga hatua kubwa katika ujenzi wa bweni la wasichana katika chuo kikuu cha Al-Ameed baada ya miezi mitatu ya kufanya kazi mfululizo, ujenzi huo unafanyika ndani ya uwanja wa chuo kikuu cha Al-Ameed katika eneo lenye ukubwa wa mita za mraba (1113).

Rais wa kitengo hicho Muhandisi Abbasi Mussawi amebainisha kua: “Mradi huu umehusisha ujenzi wa jengo la chuma lenye vyumba (38) na vyoo (13) pamoja na majiko mawili na vyumba viwili vya kufulia na kumbi za kujisomea pamoja na kumbi za kulia chakula”.

Akaongeza kua: “Tumesha kamilisha uwekaji wa huduma mbalimbali za msingi kama vile; mtandao wa vyoo, mabomba ya maji, umeme, sistim ya mawasiliano ambayo imewekwa kwa kushirikiana na kitengo cha uhandisi, pia tumeweka madirisha (pvc) na kuyawekea vitu vya kupitisha hewa, vilevile tumesha piga ripu ndani ya vyumba na katika korido zote, na kuta za nje tumeweka smenti, pia tumesha weka paa la pili, tunatarajia mradi huu utakamilika hivi karibuni Insha-Allah”.

Siku za nyuma uongozi wa chuo ulisema kua: “Mradi huu ni muhimu sana kwa chuo kikuu cha Al-Ameed, kwa sababu unatekelezwa wakati ambao tunakaribia kusajili wanafunzi wa mwaka mpya wa masomo, chuo kinawapa umuhimu mkubwa wanafunzi wa kike, mwaka jana tulipokea idadi kubwa ya wasichana kutoka mikoa tofauti ya Iraq, jambo ambalo linatulazimu kujenga bweni zuri kwa ajili yao, na kuwafanya wasipate tabu ya sehemu za kujisomea, ambapo katika jengo hili kutakua na kumbi bora za kujisomea na kila kitu ni bure, hakuna malipo ya zaidi ya ada yao ya kawaida”.

Tunapenda kufahamisha kua kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu kina nafasi kubwa ya ujenzi na ukarabati wa majengo ambayo yapo chini ya Ataba tukufu, kwani kina mafundi na wabobezi wa fani mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: