Zaidi ya watu (11,000) wamefanyiwa ziara kwaniaba…

Maoni katika picha
Watu walio fanyiwa ziara ya Arubaini kwaniaba wamefika (11,751) kutoka nchi tofauti Duniani, kupitia mtandao wa kimataifa Alkafeel kwenye ukurasa wake wa ziara kwaniaba, wamefanyiwa ziara ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na swala ya ziara na dua.

Asilimia kubwa ya watu walio jisajili katika ziara hii -ambayo usajili ulianza siku kumi kabla ya ziara- wanatoka katika nchi zifuatazo: (Iraq, Baharain, Saudia, Yemen, Qatar, Kuwait, Sirya, Lebanon, Tunisia, Misri, Swiden, Denmak, Norwey, Namsa, Marekani, Kanada, Finlendi, Jodan, Ungereza, Krashia, Tashik, Afghanistani, India, Pakistani, Uturuki, Iran) pamoja na nchi zingine.

Baada ya kumaliza kufanya ziara hii tukufu tumeelekea katika mji wa Amirul Mu-uminina (a.s) katika kaburi lake tukufu na kufungua mlango wa ziara katika kumbukumbu ya kifo cha ndugu yake mtoto wa Ammi yake Mtume Mtukufu (s.a.w.w), mtandao unatoa wito kwa waumini wote duniani wasajili majina yao kwa ajili ya kufanyiwa ziara kwaniaba, kwani hii ni miongoni mwa ziara maalumu zilizo himizwa na Maimamu wa Ahlulbait (a.s) na wapenzi wao, wajisajili kupitia anuani ifuatayo: (https://alkafeel.net/zyara/).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: