Kupitia hamla kubwa: Kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu chashiriki kusafisha mji mkongwe baada ya kumaliza ziara ya Arubaini…

Maoni katika picha
Kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu kimeshiriki katika kazi ya kusafisha mitaa ya mji mkongwe wa Karbala hususan maeneo ya karibu na haram mbili tukufu, wameshiriki kwa wingi wakiwa na vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi, wameondoa taka zote zilizo kuwa kwenye mapipa ya taka pamoja na kusafisha maeneo yeto yaliyo kaliwa na mawakibu katika kipindi cha ziara ya Arubaini.

Rais wa kitengo hicho Bwana Adnani Ni’mah amebainisha kua: “Hakika ushiriki huu ni sehemu ya mkakati uliowekwa na kitengo hiki katika ziara ya Arubaini, mkakati huo haukuishia mwisho wa ziara, unaendelea hadi baada ya ziara, watumishi wetu wanashiriki kwa ukamilifu katika kazi ya usafi, kazi hii imehusisha eneo la katikati ya haram mbili tukufu na barabara zinazo zunguka eneo hilo pamoja na barabara zinazo elekea katika Ataba mbili tukufu, pamoja na baadhi ya mitaa ya mji mkongwe”.

Akabainisha kua: “Ndani ya muda mfupi tumeweza kurejesha muonekano wa eneo la katikati ya haram mbili tukufu katika hali yake ya kawaida, kutokana na juhudi za watumishi wa eneo la katikati ya haram mbili za kudumisha usafi na kulinda utukufu wa eneo hili”.

Kumbuka kua kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu kilicho chini ya Ataba mbili tukufu Husseniyya na Abbasiyya ni sawa na vitengo vingine vya Ataba hizo, kimefanya kila kiwezalo katika kuhakikisha kinatoa huduma bora kwa mazuwaru wa Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kumbukumbu ya Arubaini ambayo imehudhuriwa na mamilioni ya watu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: