Kitengo cha habari na utamaduni chatangaza kufanikiwa kwa mkakati wake wa vyombo vya habari katika ziara ya Arubaini na chasisitiza kua matangazo yake yalinufaisha makumi ya vituo vya luninga…

Maoni katika picha
Kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza mafanikio ya mkakati wake wa vyombo vya habari katika ziara ya Arubaini, katika aina zote za vyombo vya habari, redio, machapisho, luninga pamoja na mitandao ya kielektronik, zaidi ya vyombo vya habari (240) vimeshiriki kutangaza matukio ya zaira hii.

Kwa mujibu wa maelezo ya makamo rais wa kitengo hiki, Sayyid Aqiil Abdulhussein Yasiriy, amesema kua: “Kabla ya siku chache kuanza ziara tulifanya vikao na idara zinazo husika moja kwa moja na habari, na kujadili mkakati wa utangazaji wa ziara ya Arubaini, katika vikao hivyo tulikubaliana kuandaa mkakati wa matangazo unao endana na vifaa tulivyo navyo, na utakao wezesha kutangaza tukio hili kimataifa, tukio ambalo kadri vyombo vya habari vinapo kutana na kulitangaza bado havilitendei haki”.

Akabainisha kua: “Kituo cha kuandaa vipindi na matangazo ya moja kwa moja Alkafeel kilikua na nafasi kubwa katika mkakati huu, kiliandaa masafa ya matangazo ya moja kwa moja (mubashara) ya bure katika ziara ya Arubaini, ambayo ilitumika kurusha matembezi ya Arubaini kuanzia miji ya mbali hadi Karbala, na kurusha matukio ya kuomboleza ndani ya malalo mawili matukufu pamoja na mawakibu za kuomboleza, na kurusha vipande vya video za waombolezaji zilizo tengenezwa siku za nyuma, huduma hiyo imenufaisha makumi ya vyombo vya habari vya ndani na nje ya Iraq, luninga zilizo shiriki mwaka huu zinazidi idadi ya luninga zailizo shiriki mwaka jana, kutokana na uzowefu walionao wataalamu wetu pamoja na vifaa vya kisasa vilivyopo kituoni, hivyo kuweza kutoa picha zenye ubora mkubwa zinazo endana na luninga zenye ubora mkubwa (Clean) na zinazo kidhi mahitaji ya wateja, kwa hiyo vituo vingi vilivutiwa kurusha matukio ya ziara hii inayo hudhuriwa na mamilioni ya watu”.

Akafafanua kua: “Kuhusu upande wa redio Idhaa ya Alkafeel ilikua na nafasi kubwa katika kutangaza matukio ya ziara hii, ilitangaza matukio na mazingira halisi ya ziara na kumfanya msikilizaji atambue vizuri mazingira ya ziara, kuhusu machapisho, machapisho ya Alkafeel na Alkhamisi yaliyo gawiwa bure kwa maelfu ya mazuwaru yalichukua nafasi kubwa ya kuwajulisha mazuwaru mambo yanayo husiana na ziara ya Arubaini, na kuhusu mitandao ya kielektonik, mtandao wa kimataifa Alkafeel nao ulichukua nafasi kubwa ya kutangaza matukio mbalimbali ya ziara hii, ulianza kutangaza mambo yanayo husiana na ziara hii tangu siku za mwanzo, na ulianza kutangaza mazuwaru wakiwa miji ya mbali na Karbala hadi walipo fika Karbala, pamoja na kuandika harakati zinazo fanywa na vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu na huduma inazo toa kwa mazuwaru, sambamba na kurusha picha nyingi bila kusahau mradi ulioanzishwa na kundi la waandishi wa habari ulio pewa jina la (kwa macho yao)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: