Maahadi ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu: Zaidi ya walimu (600) wa Qur’ani waliwekwe katika vituo (200) vya ufundishaji wa usomaji sahihi kwa mazuwaru wa Arubaini…

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Atabatu Abbasiyya imetangaza kua zaidi ya walimu wa Qur’ani (600) ambao wapo chini ya matawi ya Maahadi hiyo, pamoja na walimu wa kujitolea, wameshiriki kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani katika vituo (200) kwenye mikoa tofauti katika barabara zinazo elekea Karbala, miongoni mwa mikoa hiyo ni Bagdad, Muthanna, Najafu, Baabil na wilaya ya Hindiyya, pamoja na makao makuu ya mji mtukufu wa Karbala sanjari na vituo vilivyo funguliwa ndani ya uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), mazuwaru walikua wanafundishwa usomaji sahihi wa Qur’ani kwa kutumia folda zenye machapisho yanayo bainisha maeneo ambayo hukosewa na watu wengi katika usomaji ambayo ni haraka na matamshi ya herufi katika usomaji wa Qur’ani na baadhi ya adhkaar, zaairu alikua anasoma kama anavyo soma anapokua katika swala kisha mwalimu anamsahihisha sehemu atakazo kosea na kumfundisha matamshi sahihi.

Maahadi imebainisha kua; asilimia kubwa ya wanufaika ni watu wenye umri mdogo na wale ambao hawakupata nafasi ya kumaliza masomo yao, pamoja na wageni wasiojua kiarabu, walio kuja Karbala kutoka nchi mbalimbali duniani.

Kumbuka kua Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, miongoni mwa mikakati yake katika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), ni kuweka vituo vya kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu katika sura fupi ambazo husomwa mara nyingi ndani ya swala, ukizingatia kua swala ni nguzo ya Dini, ikikubaliwa na ibada zingine zinakubaliwa na ikikataliwa na ibada zingine zinakataliwa, kwa hiyo walijikita zaidi katika kufundisha swala sahihi hususan swala za faradhi na sunna ikiwa ni pamoja na usomaji wa surat Fat-ha, Ikhlasi na Kauthara kwa kua kuna idadi kubwa ya mazuwaru ambao hawawezi kuzisoma sura hizo au wanazisoma kimakosa na kufanya nguzo muhimu ya swala isikamilike, mazuwaru waimeshukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia maahadi ya Qur’ani inayo toa chakula cha roho kwa waumini, ukiwemo mradi huu muhimu wa kusomesha usomaji sahihi katika swala ambao ni sharti la kusihi kwa faradhi hiyo tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: