Mwendelezo wa machapisho yaliyo hakikiwa: Kituo cha kimataifa Al-Ameed chatoa jarida (kitabu) cha mtiririko wa khutuba za Ijumaa…

Maoni katika picha
Kituo cha kimataifa Al-Ameed chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu katika mfululizo wa kuhakiki khutuba za Ijumaa, kimetoa kitabu (juzuu la pili na la tatu) kilicho kusanya khutuba za Ijumaa za mwaka (2005m/ 1425-1426h), kitabu ambacho kitakua ni marejeo ya wanafunzi wa elimu za juu na watafiti.

Rais wa kitengo cha vitabu (mausuaat) katika kituo cha kimataifa Al-Ameed Dokta Kariim Hussein Naasih Alkhalidi amebainisha kua: “Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu tunatoa kitabu hiki cha khutuba za Ijumaa zilizo tolewa na wanachuoni ambao ni wawakilishi wa Marjaa Dini mkuu na manaibu wao katika mwaka wa (2005m), mwaka wenye matukio mengi makubwa na mabadiliko mengi hapa Iraq, wakati wa uvamizi wa nchi za kigeni zilizo andika katiba inayo lenga kufuta misingi ya uislamu na kuweka viongozi ambao ni vibaraka wa nchi za magharibi, Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu alisimama imara dhidi ya njama hizo, Mheshimiwa Ayatullahi Sayyid Ali Husseini Sistani alikua anafahamu njama zinazo pangwa na wavamizi wa kimarekani, khutuba za wawakilishi wake zikawa zinalingania uzalendo na uislamu, kwa ajili ya kuhakikisha taifa linaendelea kulinda misingi mitukufu ya uislamu na kulinda umoja wa waislamu wa Iraq”.

Akaongeza kusema kua: “Khutuba za Ijumaa zilizo tolewa mwaka (2005m) katika mji wa Karbala, zinaonyesha uwelewa wa Marjaa Dini mkuu wa mambo yatakayo tokea baadae, kwa hiyo khutuba zilijikita katika kuelimisha mambo ya kisiasa, kiuchumi pamoja na mambo ya kiitikadi hasa katika khutuba za kwanza katika kila mwezi, kwa kutoa kitabu hiki tunatarajia kuweka mikononi mwa wasomaji na walimu wa vyuo vikuu na wanafunzi wao mada nyingi muhimu; khutuba hizi zinaelezea kipindi muhimu katika historia ya Iraq kitakacho kumbukwa miongo na miongo.

Kumbuka kua miongoni mwa vitabu vya kielimu vilivyo tolewa na kituo cha kimatifa Al-Ameed chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya ni (kitabu cha khutuba za Ijumaa), baada ya kuhakikiwa na kutimiza vigezo vya kielimu, na kua marejeo ya wanafunzi wa elimu za juu na watafiti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: