Shule za Al-Ameed zaanzisha tawi jipya…

Maoni katika picha
Baada ya kupatikana mafanikio makubwa katika shule za Al-Ameed na kutokea msongamano wa wanafunzi katika shule hizo, kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimeamua kufungua shule mpya kwa ajili ya kupokea idadi kubwa zaidi ya wanafunzi, limezinduliwa jengo jipya la shule ya upili (sekondari) ya wavulana Sayyid Almaa karibu na jengo la Durra, lenye ubora mkubwa unao endana na wanafunzi wanao omba kujiunga na shule.

Mwalimu mkuu wa shule Ustadh Muslim Ghanimiy amesema kua: “Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu tumefanikiwa kuhamisha sekondari ya Sayyid Almaa ya wavulana kutoka barabara ya Sanaatir hadi sehemu mpya katika majengo ya Durra hapa Karbala”, akafafanua kua: “Shule ina ubora mkubwa; kuanzia ukubwa wa eneo lake, vyumba vya madarasa ni vikubwa vina uwezo wa kuingia wanafunzi wengi, na vimewekwa vifaa vya kusomea vya kisasa, kama vile screen za kisasa, mbao za kisasa, pamoja na kuwepo kwa mazingira bora ya kujisomea na maabara yenye vifaa vyote muhimu kwa ajili ya masomo ya fizikia, kemia, sayansi na mengineyo pia kuna kompyuta za kutosha, shule ina uwanja mkubwa wa michezo mbalimbali ambayo husaidia kukuza uwezo wa akili za wanafunzi”, akasema kua: “Shule imeandaa magari yenye viyoyozi kwa ajili ya kupeba wanafunzi kuwatoa na kuwarudisha makwao”.

Akabainisha kua: “Kuhamia katika jengo jipya kunatokana na ongezeko kubwa la wanafunzi, lililo sababisha ufanyike upanuzi wa jengo na madarasa ya sekondari kwa ajili ya kupokea idadi kubwa ya wanafunzi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: