Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu chatangaza kufanikiwa kwa mkakati wake katika ziara ya Arubaini na chasema maelfu ya mazuwaru wamenufaika…

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kufanikiwa kwa mkakati wake katika ziara ya Arubaini, katika ratiba ya tablighi, utamaduni na maelekezo, wakasisitiza kua maelfu ya mazuwaru wamenufaika na huduma zao zilizo kua zinatolewa katika vituo walivyo fungua kwenye barabara zinazo elekea Karbala na ndani ya uwanja wa haram tukufu, pamoja na majengo ya kutoa huduma yaliyo chini ya Ataba na mawakibu Husseiniyya.

Kitengo kimefafanua kua shughuli zake zilikua ni:

  • - Kuweka vituo vya tablghi kwa ajili ya kujibu maswali ya mazuwaru wanao kwenda kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kuna walio jibiwa mmoja mmoja na walio jibiwa kwa vikundi katika mradi wa tablighi za wanahauza.
  • - Kugawa kwa maelfu ya machapisho yenye maelekezo na mafundisho ya Dini kwa mazuwaru.
  • - Kuswalisha swala za jamaa katika majengo ya kutoa huduma yaliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu na katika uwanja wa haram.
  • - Kujibu maswali ya mazuwaru wanaokuja katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ndani ya ofisi ya kitengo muda wote.
  • - Kutoa mihadhara ya Dini ndani ya uwanja mtukufu wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na katika barabara zinazo tumiwa na mazuwaru wengi pande zote za mji wa Karbala.
  • - Kusambaza mubalighina katika mawakibu za kutoa huduma kwa ajili ya kuwapa maelekezo na mawaidha.
  • - Kuzungumza katika luninga na redio kwa ajili ya kufafanua malengo ya ziara ya Arubaini.
  • - Kuweka hadithi zinazo elezea malengo ya ziara ya Arubaini katika screen za nje.
  • - Kusambaza matangazo yenye mwanga yanayo elekeza baadhi ya mambo muhimu kwa mazuwaru, na mambo muhimu yanayo husiana na ziara ikiwa ni pamoja na adabu zake.

Fahamu kua kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu ni miongoni mwa vitengo vyenye uhusiano wa moja kwa moja na watu wanaokuja kumzuru Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa sababu kinahusika na kumuandaa kiroho zaairu na kubainisha malengo ya ziara, na kufafanua kila jambo kubwa na dogo, ili kumuwezesha kutambua malengo muhimu yaliyo kusudiwa na Imamu Hussein (a.s), na kuwafanya mazuwaru wanufaike nayo na waweze kupambana na dhulma kila sehemu duniani, na sio kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) peke yao, bali kwa wafuasi wa kila Dini, na haya ndio mapinduzi ya Husseiniyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: