Siku ya kesho Juma Tano, ni siku ya kumbukumbu ya msiba mkubwa katika umma wa kiislamu, tarehe kama ya kesho (mwezi 28 Safar) ni siku ya kifo cha Muokozi wa Umma Mtume Muhammad (s.a.w.w), ni siku ya kuhuisha msiba huo mkubwa na kuwapa pole Ahlulbait (a.s), makundi ya waombolezaji yanaelekea katika kaburi la Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s) katika mji wa Najafu, kumpa pole kwa kifo cha ndugu yake na mtoto wa Ammi yake Mtume wa rehma Muhammad (s.a.w.w).
Baadhi ya waumini wanatembea kwa miguu kuelekea katika mji wa Najafu Ashrafu, wameshuhudiwa maelfu ya waumini wanao tembea kwenda Najafu kutoka ndani na nje ya Iraq, kwenda kumpa pole Amirul Mu-uminina Ali bun Abu Twalib (a.s) tangu siku mbili zilizo pita.
Makundi ya waumini hao wanajikumbusha msimamo wake wakati anafikisha ujumbe wa uislamu kwa walimwengu, mji wa Najafu umejiandaa kupokea makundi makubwa ya mazuwaru wa Imamu Ali (a.s), taasisi za serikali na binafsi jimejipanga kutoa huduma zote muhimu kwa mazuwaru, askari wa mji wa Najafu wameimarisha ulinzi kufuatia ziara hii.
Mawakibu Husseiniyya zimefunga hema katika marabara zote zinazo elekea katika mji wa Najafu kwa ajili ya kuwahudumia mazuwaru wa Amirul Mu-uminina (a.s), ukizingatia kua maukibu nyingi zilizo kwenda Najafu ni zile zilizo kua zinatoa huduma kwenye ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) katika mji wa Karbala, wametoa hema zao katika mji wa karbala na kuhamia katika barabara zinazo kwenda Najafu.
Kumbuka kua kifo cha Mtume wa mwisho Muhammad bun Abdillahi (s.a.w.w) kilikua mwezi (28 Safar) mwaka wa (11) hijiriyya, alikufa akiwa na miaka (63), wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wanaelekea katika kaburi la simba wa Mwenyezi Mungu Ali bun Abu Twalib (a.s) kumpa pole kufuatia kifo cha ndugu yake na mtoto wa Ammi yake Mtume wa rehma Muhammad (s.a.w.w) na hii ni miongoni mwa ziara makhsusi.