Kumbukumbu ya kifo cha Mtume na muongoaji wa umma: Wingu la huzuni latanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu…

Maoni katika picha
Mwezi wa Safar umekataa kuisha ispokua uishe kwa kutupa huzuni nyingine kubwa inayo kamilisha msimu wa huzuni na maombolezo, unatuaga kwa msiba mkubwa zaidi katika umma wa kiislamu, msiba wa kifo cha mbora wa viumbe na mwisho wa mitume, Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Kutokana na msiba huu mkubwa, kuta za Atabatu Abbasiyya tukufu zimevua vazi jeusi la Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) na kuvaa vazi rasmi la kukumbuka kifo cha babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu Abu Zaharaa Muhammad (s.a.w.w).

Kuta na nguzo za ukumbi mtukufu wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) zimefunikwa vitambaa vyeusi vilivyo andikwa maneno yanayo maanisha huzuni kutokana na msiba huu mkubwa katika nyoyo za waumini,
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: