Maukibu ya uombolezaji ya pamoja: Watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya watoa pole wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi katika kumbukumbu ya kifo cha Mtume (s.a.w.w)…

Maoni katika picha
Mwambie asiye kuwepo chini ya mbingu *** kama unasikia sauti yangu na wito wangu.

Nimepatwa ni misiba lau kama misiba hiyo *** ingeupata mchana ungegeuka na kua usiku.

Kama mwezi ukibaki katika usiku wake *** utatuweka katika tawi na kubaki hadi asubuhi.

Itakua vipi kwa aliyenusa udongo wa Ahmadi *** asiendelee kunusa wakati woto.

Ewe kipenzi cha roho zetu tumepata msiba mkubwa utokanao na wewe, wahyi umekatika na tumekukosa, hakika sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.

Kwa roho zilizo jaa huzuni na macho yanayo toka machozi, baada ya Adhuhuri ya leo (28 Safar 1440h) sawa na (7 Novemba 2018m) yamefanyika matembezi ya kuomboleza ya pamoja, na watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kwa ajili ya kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kuomboleza kifo cha Mtume mtukufu Abu Qassim Muhammad (s.a.w.w).

Matembezi yalianzia katika uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakapitia katika uwanja wa katikati ya harama mbili tukufu, wakati wa matembezi hayo walikua wanaimba kaswida zilizo amsha hisia za huzuni na kuonyesha ukubwa wa msiba katika nafsi za waumini, walipo wasili katika uwanja wa haram ya bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein (a.s), walipokewa na ndugu zao watumishi wa Atabatu Husseiniyya tukufu, na kufanya majlis ya pamoja ndani ya uwanja wa haram ya Imamu Hussein (a.s), ambapo zilisomwa kaswida na mashairi mbalimbali kuhusu Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Kumbuka kua waislamu kila sehemu ya Dunia wanaomboleza kifo cha mbora wa viumbe na hitimisho la Manabii na Mtume Muhammad (s.a.w.w), aliye fariki mwezi ishirini na nane Safar mwaka wa (11) hijiriyya, akiwa na umri wa miaka sitini na tatu, alikufa na kuzikwa katika mji wa Madina Munawwara.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: