Mwaka wa tatu mfululizo: Maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu inashiriki katika maonyesho ya kielimu na kiutamaduni ya Twafu awamu ya kumi…

Maoni katika picha
Kwa ushiriki wa maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia vituo vyake kwa mwaka wa tatu mfululizo, Asubuhi ya Juma Tano ya leo (28 Safar 1440h) sawa na (7 Novemba 2018m) maonyesho ya Twafu awamu ya kumi yameanza katika chuo kitivo cha Adabu ndani ya chuo kikuu cha Mustanswariyya chini ya anuani isemayo (Twafu ni kilele cha kujitolea na wino wa ushindi), yamepata mahudhurio makubwa ya watafiti na wasomi wa sekula kutoka nchi tofauti pamoja na viongozi wa taasisi mbalimbali na watu mashururi.

Katika mazungumzo ya mkuu wa kituo cha Makhtutwaat msaidizi, Ustadh Kamali Abdulhamidi amesema kua: “Kituo cha Makhtutwaat chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya kinashiriki kwa mara ya tatu mfululizo katika kongamano hili la Twafu, lengo la kushiriki ni kubadilishana uzowefu na kuonyesha tulicho nacho katika sekta hii pamoja na kazi tunayo fanya ya kutengeneza Makhtutwaat”.

Akaongeza kua: “Kuwepo kwetu na kushiriki katika maonyesho haya yatakayo chukua siku mbili ni kwa ajili ya kubainisha miradi ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Ataba tukufu, ukiwemo mradi wa kulinda matokeo ya kielimu ya Iraq na miradi mingine mbalimbali”.

Akafafanua kua: “Tumepata maswali mengi kutoka kwa walimu na wanafunzi wanao tembelea maonyesho haya, tumewajibu na kutoa ufafanuzi zaidi pale ulipo hitajika, tuna mshukuru Mwenyezi Mungu mtukufu ushirikiano ni mzuri sana, tunatarajia kupanua ushirikiano zaidi katika miaka ijayo”.

Mkuu wa kitivo cha adabu Dokta Farida Jaasim amesema kua: “Maonyesho haya yamehusisha vitu vingi ikiwa ni pamoja na majadiliano mbalimbali sambamba na kuonyesha filamu ninazo fafanua ushindi wa raia wetu na jeshi pamoja na Hashdi dhidi ya makundi ya kigaidi”.

Akaongeza kusema: “Awamu hii imeshuhudia majadiliano ya aina mbalimbali, na yamefanyika kwa kutumia zaidi ya lugha moja, hakika ni majadiliano ya pekee katika chuo kikuu cha Mustanswariyya, yamekua tofauti na majadiliano yaliyo pita kwa sababu yanaelezea ushindi ulio patikana pamoja na maarifa ya utamaduni, na tumekaribisha idadi kubwa ya taasisi za serikali na wizara”.

Akabainisha kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu inanafasi kubwa katika kongamano hili ambapo inashiriki kwa mwaka wa tatu mfululizo kupitia kitengo chake cha habari na utamaduni”.

Tunapenda kufahamisha kua Maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu imesha shiriki mara nyingi katika makongamano ya kitaifa na kimataifa, ikiwa ni pamoja na kongamano la filamu lililo fanyika kwa mara ya kwanza kimataifa, pia inamiradi mingi inayo saidia ukuwaji wa elimu ya maktaba, kama vile mradi wa kulinda matokeo ya kielimu ya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: