Atabatu Abbasiyya tukufu yamaliza kazi katika moja ya miradi mikubwa ya maji safi na salama ya kunywa katika mkoa wa Karbala…

Maoni katika picha
Baada ya mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu kufanya kazi miezi tisa mfululizo mchana na usiku katika mradi mkubwa wa maji safi na salama ya kunywa kwenye mkoa mtukufu wa Karbala (kituo cha maji cha Khairaat), leo wametangaza kumaliza kazi za mradi huo uliotekelezwa kwa ushirikiano na Atabatu Husseiniyya tukufu pamoja na ofisi ya maji ya Karbala, sasa kinazaliza (m 31400/saa) wakati awali kilikua kinazalisha (m 3200/ saa), mradi huu utamaliza tatizo la maji katika vijiji vilivyo kua na tatizo hilo pamoja na mawakibu Husseiniyya ambazo hujaa katika barabara ya (Yaa Hussein).

Kwa mujibu wa maelezo ya Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi ambaye ni rais wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya amesema kua: “Mradi wa kituo cha maji cha Khairaat ambacho kwa sasa kinaitwa (Mradi wa maji ya Alkafeel) unao tekelezwa katika eneo lenye ukubwa wa mita za mraba (1150), ni miongoni mwa miradi inayo wagusa moja kwa moja wananchi wa Karbala iliyo fadhiliwa na kugharamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akabainisha kua: “Mradi huu umeboreshwa na kuongezewa vituo vinne ambavyo vimesaidia kuinua kiwango cha uzalishaji wa maji hadi kufikia (m 31400/saa), pamoja na kuweka mabomba ya urefu wa (km 21) kutoka kwenye mradi wa Khairaat katika mji wa Sajlah na Fiyadah (miji iliyopo kusini mwa mkoa) hadi katika mji wa Zubailiyya, sambamba na kuweka bomba zingine zenye urefu wa (km 13) kwa ajili ya kugawa maji kwa mawakibu Husseiniyya katika barabara ya (Labbaika ya Hussein) pamoja na majengo ya kutoa huduma ambayo yapo chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya”.

Akafafanua kua: “Mradi huu ulitanguliwa na ujenzi wa eneo la kufunga mitambo ya kusukuma maji pamoja na vifaa vyake, sambamba na kukarabati sehemu zilizo kua zimeharibika na kuhakikisha eneo lote limekamilisha vigezo vya kihandisi vinavyo takiwa katika miradi ya aina hii”.

Fahamu kua mradi huu utapunguza tabu ya maji safi na salama ya kunywa kwa wakazi wa maeneo tajwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: